Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKENDA AZINDUA KITUO MAHIRI CHA USAMBAZAJI TEKNOLOJIA ZA KILIMO




Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akizungumza mara baada ya kuzinduliwa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma, leo, Septemba 24, 2021. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)





Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda (katikati) akipata malezo kutoka kwa Mratibu wa Utafiti mazao jamii ya Mikunde, Meshack Makenge juu ya mbegu bora za zao la alizeti zinazotoa mafuta mengi zaidi zinazozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) mara baada ya kuzinduliwa kwa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma, leo, Septemba 24. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk Geofrey Mkamilo (kushoto).
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwa Watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) juu ya mbegu za zao la ndizi wakati akiwa katika kitalu cha zao hilo katika Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma mara baada ya kufungua kituo hicho, leo, Septemba 24, 2021.

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda (kulia) akimskiliza Mtaalam wa mazao ya Mtama, Ulezi na Uwele kutoka Dkt Robert Simbagige kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), kituo cha Hombolo juu ya mbegu bora za zao la ulezi zinatengenezwa na kituo hicho mara baada ya uzinduzi wa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma, leo, Septemba 24, 2021

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akikata utepe kuzindua Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni, kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Jijini Dodoma leo, Septemba 24, 2021.

Sehemu ya Washiriki wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwa Watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Nzuguni jijini Dodoma mara wakati akifungua kituo mahiri cha usambazaji teknolojia za kilimo, leo, Septemba 24., 2021.

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwa Watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) juu ya mbegu za zao la ndizi wakati akiwa katika kitalu cha zao hilo katika Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma mara baada ya kufungua kituo hicho, leo, Septemba 24, 2021.




Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akizungumza mara baada ya kuzinduliwa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni jijini Dodoma, leo, Septemba 24, 2021.




Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma






Changamoto kubwa ya wakulima nchini ni pamoja na kutotumia mbinu za kilimo bora kama vile kutotumia mbegu bora, kutozingatia nafasi kati ya mmea na mmea, kutotumia mbolea kwa usahihi na matumizi hafifu ya viuatilifu.




Katika kukabiliana na changamoto hiyo serikali imeanzisha kituo mahiri kitakachowasaidia wakulima kuongeza ufahamu wa kanuni za kilimo bora kwa wadau hususani wakulima na kuongeza ushirikiano kati ya wakulima, wagani, watafiti na wadau wa mbegu.




Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 24 Septemba 2021 wakati akizindua Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo kilichopo Nzuguni, kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Jijini Dodoma.




Amesema kuwa kituo hicho kimeanzishwa muda muafaka wakati Wizara ya Kilimo imeweka mkakati wa kuimarisha huduma za ugani nchini.




Waziri Mkenda ametoa rai kwa viongozi wa mikoa iliyo katika kanda ya kati kukitumia kituo hicho kuwajengea uwezo kwa vitendo maafisa ugani ili wasaidie kuwajengea uwezo wakulima katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza uzalishaji na tija, kuchangia kuwa na uhakika wa chakula, kipato, lishe bora na ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla.




Amesema kuwa kituo hicho mahiri cha kusambaza teknolojia za kilimo kilichopo kwenye viwanja vya maonesho vya Nzuguni Jijini Dodoma kitatoa mafunzo ya matumizi ya teknolojia za kilimo bora kama vile matumizi ya mbegu bora, kupanda kwa nafasi pamoja na matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu.




Waziri Mkenda ameongeza kuwa "Matarajio yangu kituo hiki kitakuwa chachu ya kuwaunganisha wadau wa kilimo na masoko, pia kuanzisha kanzidata ya masoko ya mazao mbalimbali"




"Nawasihi viongozi wa Halmashauri zote kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuli za uhaulishaji/usambazaji wa teknolojia bora za kilimo na kuimarisha huduma za ugani nchini" Amesisitiza Waziri Mkenda




Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dodoma Mhe Riziki Lulida pamoja na kumpongeza waziri wa Kilimo lakini pia ameiomba serikali kuhimiza mikakati ya uzalishaji wa alizeti kwa wingi kwa kutoa fedha za mikopo kwa wanawake na hususani wakulima ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo.




Mhe Lulida amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa katika kuwanufaisha wafanyakazi wa serikali na kutambulika hivyo inapaswa kuongeza msisitizo wa kuwapatia vitendea kazi na kuwatambua maafisa ugani kutokana na kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa manufaa ya wakulima wote nchini.




Awali, akitoa taarifa ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini- TARI Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Dkt Geofrey Mkamilo amesema kuwa njia pekee ya wakulima kuongeza kipato ni pamoja na kuzingatia taratibu zote za kilimo ikiwemo kupata mafunzo ya kilimo yanayotolewa katika vituo 17 vya utafiti wa kilimo vilivyopo nchini.




Amesema kuwa TARI imekuja na mkakati wa kuhakikisha kuwa wakulima wanaelimishwa kuhusu matumizi ya zana bora za kilimo, kupanda kwa kufuata taratibu elekezi zinazotolewa na wataalamu ikiwemo kujifunza teknolojia sahihi zitakazoleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo.




MWISHO

Post a Comment

0 Comments