Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATENGA BIL 2.2 KUNUNUA MBEGU ZA ALIZETI


******************

Na Doreen Aloyce,Dodoma.

ILI kupunguza uhaba wa mafuta nchini na kuinua Sekta ya kilimo Cha Alizeti Serikali imetenga shilingi bilion 2.2 kwa ajili ya kuandaa mbegu bora za Alizeti.


Hayo yamesemwa Leo Jijini hapa na Waziri wa Kilimo Profesa Aldof Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa Habari amesema walipanga kupata tani 5,000 lakini wamefanikiwa kupata tani 1600 za mbegu hizo. 


Aidha amesema hii ni mara ya kwanza Serikali imetekeleza suala la mbegu hivyo kila mmoja lazima apate mbegu hizo kwa sababu ni bei rahisi. 


"Mbegu hizi zitakuwa zinapatikana katika halmashauri na kwa bei rahisi ili kuokoa fedha zinazotumika kwa ajili ya kununua mafuta, "amesema Profesa Mkenda..


Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha mwakani hawaagizi tena mbegu nchini Ufaransa,wanahitaji kuona mbegu bora zinapatikana hapa nchini. 


Amesema Serikali imekuwa ikitumia sh nusu trion kila mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta jambo ambalo halikubaliki kabisa wanahitaji kuona mafuta yanapatikana hapa nchini. 


Amefafanua zaidi kuwa wameteua mikoa mitatu ambayo italima alizeti chini ya usimamizi mzuri ili yaweze kuzalisha mbegu za alizeti Mikoa hiyo na wilaya zake wamegawana ekari kwa ajili ya kulima zao hilo katika mikoa hiyo. 


Profesa Mkenda amegawa mbegu kwa Wakuu wa Wilaya ambapo zitapelekwa katika halmashauri kwa ajili ya kwenda kuwauzia wananchi ambao ni wakulima. 

Mbali na hilo amesema wameongeza fedha za mafunzo kwa maafisa ugani na mabwana shamba ili waweze kuwapa maelekezo mazuri wakulima. 


Amesema wameongeza Ekari kutoka sh milion 16 hadi bilion 11 kwa ajili ya kuwapa mafunzo maafisa ugani na mabwana shamba wote ili wawe na ujuzi. 


Mbali na hilo amesema watazidi kuyapa kipaumbele mazao ya Pamba, Michikichi, Karanga na mengine ili kumaliza uhaba wa mafuta nchini.


Naye Katibu Tawala wa Mkoa Dk Fatma Mganga alisema wetenga ekari 800,000 kwa mkoa wa Dodoma ambapo kila Wilaya itapata ekari zake kwa ajili ya kupanda mbegu hizo.


Amesema tayari wilaya zimeshapewa ekari za kulima ambapo mbegu hizo zitapatikana katika halmashauri mbalimbali hapa jijini Dodoma. 


Hata hivyo amempongeza Waziri Profesa Mkenda kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ajili ya kuinua Kilimo cha alizeti hapa nchini. 


Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Bahi ambae alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,Mwanahamisi Mkunda alimuhakikishia Waziri wa Kilimo kuwa mbegu hizo zitatumzwa vizuri na wakulima wote watazipata 


Alisema kilio cha wakulima wa Alizeti kitazidi kukua hapa nchini. 


Naye Mkulima Stephen Marriale kwa niaba ya wakulima wenzake ameishukuru serikali kwa hiki walichokifanya na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali sekta ya Kilimo.

Post a Comment

0 Comments