Ticker

6/recent/ticker-posts

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUACHA KUTUMIA VILEVI KUWAKINGA WATOTO WANAOZALIWA
***********************Na Doreen Aloyce, Dodoma

IMEELEZWA kuwa mama wajawazito hapa nchini wanaotumia vilevi hasa pombe wamekuwa chanzo Cha kuwasababishia watoto wanaozaliwa kuwa na matatizo yabafya ya akili jambo ambalo sio sahihi na hatarishi kwa maisha yao.
Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akili katika Hospitali ya Taifa ya magonjwa ya Akili Mirembe Dkt.Innocent Mwombeki wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya Habari Jijini Dodoma Ikiwa ni kuelekea Oktoba 10 ambayo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani.
Aidha amesema kuwa mama mjazito anapaswa kutambua kuwa anapokunywa pombe anamuweka hatarini mtoto atakayezaliwa kuwa na matatizo hayo kwani kumsababishia athari katika ukuaji wa ubongo kwa mtoto aliye tumboni na hivyo kumsababishia tatizo la afya ya akili pindi atakapozaliwa.
Alibainisha kuwa kama Serikali inapaswa kuangalia ongezeko la watu wenye matatizo ya afya ya akili,kwa kuangalie tangu mtoto anapokuwa tumboni Kwani wapo akina mama wengi wanatumia vilevi wanapokuwa wajawazito bila wao kujua madhara yanayoweza kujitokeza kwao na Watoto walioko tumboni.
"Naomba kuwashauri akina mama hasa wajawazito kuacha matumizi ya vilevi na kijidanganya kuwa mnawafanya watoto kuwa na afya Bali mjitajidi ili kuwanusuru watoto walio tumboni kuzaliwa wakiwa na matatizo ya afya ya akili
"Na niwambie kwamba mama mjamzito kutumia vilevi inasababisha ukuaji wa ubongo wa mtoto kuathirika na kusababisha mtoto kuzaliwa na matatizo ya afya ya akili na kuendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili" amesema Dkt.Mwombeki.
Dkt. Mwombeko amesema licha ya athari hizo Bado Kuna sababu nyingine inayosababisha matatizo ya afya ya akili ikiwa ni pamoja na mtoto kutolishwa vizuri tangu anapozaliwa,kufanyiwa ukatili mbalimbali ,vipigo kwa watoto na manyanyaso mbalimbali ambayo yanaweza kumuathiri mtoto.
“Pia kuna wale ambao wana vinasaba vya matatizo hayo katika ukoo,akipata changamoto kidogo tu katika maisha anajikuta anapata matatizo ya afya ya akili,lakini umasikini ,matatioz kazini yote hayo huchangia mtu kupata matatizo ya afya ya akili"amesema Dkt.Mwombeki.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Shedrack Makubi amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha watanzania milioni saba wana matatizo ya afya ya akili huku akiutaja mkoa wa Dar es salaam kuwa kinara kwa kuwa na watu wengi wenye matatizo ya afya ya akili kutokana na watu wengi matatizo hayo kwenda Jijini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Aidha watu zaidi ya milioni 300 wana matatizo ya afya ya akili duniani.
Mapema, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili Mirembe,Dkt.Paul Lawale amesema wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya hospitali hiyo kuwa chakavu kutokana na kujengwa wakati wa mkoloni miaka 95 .

Post a Comment

0 Comments