Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI MBENNAH ATETA NA MAKAMU RAIS WA JAMHURI YA MAURITIUS

Makamu Rais wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Eddy Boissezon, GOSK akiteta na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof. Emmanuel Mbennah
Makamu Rais wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Eddy Boissezon, GOSK akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof. Emmanuel Mbennah


*****************************

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof. Emmanuel Mbennah amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Rais wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Eddy Boissezon, GOSK.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wameonesha kuridhishwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo na kuahidi kuendelea ushirikiana katika sekta za uchumi, biashara utalii na uwekezaji.

Makamu huyo wa Rais pia ameiipongeza Tanzania kwa ushindi wa Bw. Abdulrazak Gurnah katika Tuzo ya Amani ya Fasihi.

Oktoba 7, 2021 Mwandishi wa riwaya nchini Tanzania Abdulrazak Gurnah alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kuhusu fasihi 2021.

Post a Comment

0 Comments