Ticker

6/recent/ticker-posts

TANESCO KUHARAKISHA MATENGENEZO YA BAADHI YA MITAMBO YAKE KUONGEZA UZALISHAJI KWA KUTUMIA GESI ASILIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw.Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea baadhi ya meneo katika Kituo cha kuzalisha umeme Ubungo leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw.Maharage Chande akitembelea baadhi ya meneo katika Kituo cha kuzalisha umeme Ubungo leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linachukua hatua za haraka kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asili hasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kupelekea kiwango cha maji katika mito na mabwawa kupungua kwa kiasi kikubwa.

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw.Maharage Chande wakati alipotembelea vituo vya kuzalisha Umeme Ubungo Jijini Dar es salaam na kuona kazi zinavyofanyika.

Amesema katika mpango wa kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia, kituo cha Ubungo kipo kwenye matengenezo na kikikamilika kitatupa 25MW za uzalishaji wa umeme.

Aidha amesema wanapanua mitambo ya Ubungo III ambao utatuongezea 112MW katika Gridi ya Taifa .

"Kwasasa tunaupungufu wa takribani 345MW kwa kiasi cha juu ambayo ni asilimia 21% ya uzalishaji wote na huwa kinabadilika kutokana na maji yanayoongezeka kuingia na kutoka ". Amesema

Amesema katika Mkoa wa Dar es Salaam kuna vituo vya kupozea umeme 27 kati ya hivyo 13 vimezidiwa kwa maana watumiaji wa umeme wameongezeka na vinahitajika kutanuliwa.

Post a Comment

0 Comments