Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA COP26 UNAOFANYIKA GLASGOW, SCOTLAND LEO TAREHE 01 NOVEMBA, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi Green Climate Fund (GCF) Yannick Glermarec mara baada ya kuzungumza nae Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Boris Johnson (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano mjini Glasgow, Scotland kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa COP26 leo tarehe 01 Novemba, 2021.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.

Post a Comment

0 Comments