Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI DKT. GWAJIMA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA ALMA


**********************

Na.WAMJW- DOM.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo tarehe 05 Novemba, 2021, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Muungano wa Viongozi wa Nchi za Afrika (ALMA) katika kupambana na Malaria, Mama Joy Phumaphi kutoka nchini Botswana. Katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, kwa pamoja wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya hususani ikiwemo kuanzisha Mabaraza ya Kutokomeza Malaria na kuanzisha viwanda vya bidhaa za afya hapa nchini zikiwemo za kupambana na ugojwa wa Malaria.

Aidha, kupitia kikao hicho Mama Joy Phumaphi amesema kuwa ALMA ipo tayari kuwekeza kwenye juhudi za serikali kutokomeza malaria.

Mbali na hayo Mama Joy Phumaphi ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa namna inavyofanya vizuri katika matumizi ya kadi ya alama juu ya mapambano dhidi ya malaria nchini.

Pia Dkt. Gwajima ameishukuru Taasisi ya ALMA kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchini.

Katika hatua nyingine Mama Joy Phumaphi amepata fursa ya kuonana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ambapo ametoa rai ya ALMA kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa Wabunge wa Tanzania katika Mapambano ya kutokomeza Malaria Tanzania (TAPAMA)

Post a Comment

0 Comments