Ticker

6/recent/ticker-posts

MATUKIO KATIKA UFUNGUZI WA MAONESHO YA 21 YA WAJASILIAMALI YA AFRIKA MASHARIKI


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) kushoto akiwa katika banda la Serikali ya Tanzania kupata maelezo kuhusu Maonesho ya 21 ya Wajasiliamali ya Afrika Mashariki. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi. Robert Gabriel Luhumbi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wwenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Peter Mathuki.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 21 ya Wajasiliamali ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 2 hadi 12 Desemba 2021.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na ujumbe wake wakielekea kwenye mabanda ya wajasiliamali wanaoshiriki kwenye Maonesho ya 21 ya Wajasiliamali ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 2 hadi 12 Desemba 2021.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb)
akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiliamali kwenye Maonesho ya 21 ya Wajasiliamali ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 2 hadi 12 Desemba 2021.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akiwa kwenye Banda la Vijana wa CCM mkoa wa Mwanza linalouza bidhaa za CCM kwenye Maonesho ya 21 ya Wajasiliamali ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 2 hadi 12 Desemba 2021.
Bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali ya juu zilizobuniwa na wajasiliamali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akiwa katika vazi la utamaduni la Sudan Kusini alilovalishwa baada ya kuwasili kwenye banda la nchi hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akikabidhiwa zawadi ya picha yake ya kuchora katika moja ya mabanda ya Watanzaia.Post a Comment

0 Comments