Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS ALHAJ DKT.HUSSEIN MWINYI AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA ALIYEWAHI KUWA MBUNGE WA JIMBO LA MPENDAE ZANZIBAR ISSA KASSIM ISSA (BAHARIA) KIJIJI KWAO UROA MKOA WA KUSINI UNGUJA.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu Sheikh Mahmoud Mussa Ngwali , baada ya kumalizika kwa sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa,(Baharia) Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, baada ya kuwekwa mwili wa marehemu, maziko yaliyofanyika katika makaburi ya familia katika Kijiji cha Pongwe Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu) BAADHI ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wakiitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Ngwali baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Kombo Hassan Ali, baada ya kumalizika kwa maziko ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja Marehemu Issa Kassim Issa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar.maziko hayo yamefanyika katika makaburi ya familia Kijiji cha Pongwe Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Abdulazazi Saleh Juma,(hayupo pichani) alipofika nyumba kwa marehemu katika Kijiji cha Uroa kutowa mkono wa pole kwa familia.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments