Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UJUMBE WA WAWEKEZAJI WA MAKAMPUNI YA TRIUMPH HOTELS GROUP IKULU ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Makampuni ya Triumph Hotels Group kutoka Nchini Misri, ukiongozwa na Mejor General Ehab Shoman Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa mahoteli hayo (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Kikosi cha KMKM Zanzibar Commodore Azana Hassan Msingiri.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mejor General Ehab Shoman Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa Mahoteli ya Triumph Hotels Group.(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu na ujumbe wake kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-12-2021, (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Kikosi cha KMKM Zanzibar Commodore Azana Hassan Msingiri.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar mgeni wake Mkuu wa Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Nchini Misri wa Makampuni ya Triumph Hotels Mejor General Ehab Shoman Mkurugenzi Mkuu wa Kanda wa Mahoteli ya Triumph, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-12-2021.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments