Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA YAFANYA KONGAMANO LA UWEKEZAJI SEKTA YA UTALII EXPO 2020 DUBAI


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akihutubia Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-La DubaiNaibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja akifurahia zawadi aliyopewa na Waziri wa zamani wa Mazingira na Maji-UAE, Dkt.Mohammed Al Kindi (hayupo pichani) kwa kuthamini mchango wake kwenye kukuza utalii Tanzania katika Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-La Dubai.

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Bi. Hafsa Mbanga akichangia mada katika Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-la Dubai. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan KijaziBaadhi ya Wanajumuiya ya Wafanyabiashara Dubai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja alipokuwa akihutubia Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-la Dubai.Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na wawekezaji kuhusu mifumo mizuri inayoruhusu uwekezaji Tanzania katika Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-la DubaiNaibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akikabidhiwa zawadi na Waziri wa zamani wa Mazingira na Maji UAE, Mhe. Dkt. Mohammed Al Kindi kwa kuthamini mchango wake katika kukuza utalii nchini Tanzania wakati wa Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-la Dubai. Anayeshuhudia ni Mwanzilishi & Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Vilabu Duniani, Dkt. Tariq Ahmed Nizami.

***********

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) amehutubia kongamano kubwa la uwekezaji katika Sekta ya Utalii leo tarehe 12 Desemba, 2021 katika hoteli ya Shangri-la iliyopo Dubai.

Akiongea katika kongamano hilo Mhe. Masanja ameeleza nia ya kongamano hilo kuwa ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania pamoja na kujenga mahusiano ya kiuwekezaji kwenye Sekta ya Utalii.

“Kuna umuhimu mkubwa kutumia fursa ya maonesho haya ya Expo 2020 Dubai kutangaza na kuelezea fursa za uwekezaji zilizopo nchini.” Mhe. Masanja amefafanua na pia amewakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye Sekta hii nchini Tanzania.

Aliongeza kuwa, nchini Tanzania kuna fursa nyingi za uwekezaji katika maeneo ya mijini na sehemu mahsusi za utalii zikiwemo maeneo kiutamaduni na kihistoria, malazi yaani hoteli za kitalii, migahawa, maeneo ya michezo ya gofi, utalii ikolojia, utalii wa kumbi za mikutano na utalii wa uwindaji.

Kongamano hili limehudhiriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi ya Diplomasia Dubai, Balozi Edwin Rutageruka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini TTB, Betrita Lyimo, Bi. Hafsa Mbanga kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara Dubai ikiwa ni sehemu ya Makongamano yaliyoandaliwa na Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai.

Post a Comment

0 Comments