Ticker

6/recent/ticker-posts

WAGANGA MKAJISAJILI KABLA 31 MACH, 2022- SERIKALI




**********

Na, WAMJW - DODOMA


Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wametakiwa kujisali, kuorodhesha wasaidizi wao, kusajili vituo, pamoja na Dawa wanazotumia kutibu wagonjwa kabla ya Machi 31, 2022.


Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti-Baraza la Tiba Asili/Mbadala Prof. Hamis Malebo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma hii leo Desemba, 07, 2021.

Prof. Malebo amesema kuendelea kufanya matibabu bila kupata kibali kutoka katika Baraza la Tiba Asili/Mbadala ni kosa kisheria.

Amesema kwa wote wanaoendelea kutoa huduma bila kusajiliwa wanatakiwa wawe wamejisajili kabla kufikia tarehe 31 machi, 2022, baada ya hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

“Nawataka waganga wote kujiepusha na vitendo vyote vinavyokinzana na Sheria, kanuni na taratibu zilizopo, ikiwa ni pamoja na kuacha kuweka mabango yanayopotosha jamii, kurusha matangazo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii bila ya kuwa na Kibali kutoka Baraza la Tiba sailing nchini.” amesema Prof. Malebo

Aidha amewataka wanaouza Dawa kiholela kama kwenye vyombo vya usafiri, nyumba za ibada, sokoni na sehemu zenye mikusanyiko kuacha tabia hiyo kwakuwa Dawa zote za Asili zitauzwa katika maduka ya Dawa yaliyosajiliwa.

Hata hivyo Prof. Malebo amewataka wanaotoa elimu za Tiba Asili/Mbadala kwenye Vituo vya Redio na Runinga nao kupata kibali kutoka Baraza.

Kwa upande wake Msajili-Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dkt. Ruth Suza amewataka waganga kuwamakini katika utoaji wa huduma sababu wanahusika moja kwa moja na Afya za wananchi.

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kupitia Mwenyekiti Prof. Malebo limepiga marufuku kuanzioa leo kuacha kurusha Matangazo yote ambayo hayajapitishwa na Baraza.

Post a Comment

0 Comments