Ticker

6/recent/ticker-posts

WATAKIWA KUFIKISHA MAFUNZO YA UIMARISHAJI AFYA KATIKA JAMII


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk.James Kengia,akizungumz wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya Waratibu wa afya ya jamii ngazi ya Mkoa kutoka Mikoa 26 na Waratibu 26 wa uimarishaji afya wa shule za Mikoa yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyofanyika jijini Dodoma.


Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby,akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo kwa Waratibu wa afya ya jamii ngazi ya Mkoa kutoka Mikoa 26 na Waratibu 26 wa uimarishaji afya wa shule za Mikoa yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyofanyika jijini Dodoma


Mratibu wa Health Promotion Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),akizungumz wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya siku tano ya Waratibu wa afya ya jamii ngazi ya Mkoa kutoka Mikoa 26 na Waratibu 26 wa uimarishaji afya wa shule za Mikoa yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyofanyika jijini Dodoma


Mmoja wa washiriki ambaye ni Mratibu wa Elimu ya Afya katika Shule za Mkoa wa Dar es salaam, Dk.Ndeniria Swai, akitoa neno la shukrani kwa waandaaji wa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mradi wa HPSS – Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC) na unaotekelezwa na Taasisi ya Uswisi ya Tropical and Public Health (Swiss TPH), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika jijini Dodoma


Washiriki wa mafunzo wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa ufungaji mafunzo kwa Waratibu wa afya ya jamii ngazi ya Mkoa kutoka Mikoa 26 na Waratibu 26 wa uimarishaji afya wa shule za Mikoa yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyofanyika jijini Dodoma

..................................................................... Na Alex Sonna, Dodoma

WAHUDUMU wa afya 52 waliopatiwa mafunzo ya uimarishaji wa afya wametakiwa kuyatumia mafunzo hayo kuelimisha jamii katika maeneo yao ya kazi ili kuleta mabadiliko chanya.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk.James Kengia ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo hayo ya siku tano ya Waratibu wa afya wa Mikoa 26 na Waratibu 26 wa uimarishaji afya wa shule za Mikoa yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii.

Mafunzo hayo yametolewa na Mradi wa HPSS – Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC) na unaotekelezwa na Taasisi ya Uswisi ya Tropical and Public Health (Swiss TPH), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Amesema wahudumu hao wanapaswa kuyabeba waliyojifunza na kuyafikisha kwenye maeneo yao jambo litakalosaidia kufikia malengo waliyojiwekea.

“Nishukuru HPSS na timu nzima ya wawezeshaji na niwatake washiriki suala hili lisiishie kwenye chumba hiki cha mafunzo, maana tumekuwa tukipata mafunzo mengi sana lakini yanaishia kwenye vyumba vya mafunzo, natoa rai kwenu kuyabeba haya na kufikisha kwenye maeneo yenu ya kazi.”

“Utekelezaji wa masuala ambayo tumekubaliana yanaenda sambamba na mipango yetu, ukiwa na mipango ambayo hai reflect yale tunayokwenda kuyafanya itakuwa ni vigumu katika utekelezaji, kwenye maeneo yetu kwasasa ni kipindi cha mipango,”amesema.

Dkt Kengia pia ametoa rai katika uandaaji wa mipango yao wahakikishe masuala ya utoaji wa elimu ya afya ya jamii yanapewa kipaumbele.

“Kwenye magonjwa yasiyopewa kipaumbele kuna eneo la uelimishaji, tuwe na namna ya kushirikiana kwenye kuelimisha kama tunavyoshirikiana kwenye mambo mengine, na tukatumia rasilimali chache na kufikia kwenye maeneo yetu,”amesema.

Aidha, amesema suala la huduma za afya ni hoja ya msingi ulimwenguni ikiwamo utoaji wa huduma za afya za msingi kwa wote.

“Afya ni haki ya msingi ya kila mwanadamu na suala la huduma za afya kwa wote lipo kwenye katiba ya Shirika la Afya Duniani (WHO), na watu hudhani suala la huduma za afya kwa wote ni bima ya afya, bali ni kuhakikisha kila mtu anapata huduma za afya katika huduma tiba, kinga, utengamao,”amesema.

Naye, Meneja Mradi wa HPSS-Tuimarishe Afya, Ally Kebby amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa kazi ambazo wamekuwa wakizifanya kwa kipindi cha miaka 10.

“Tulipewa dhamana na serikali kusaidia kuimarisha mfumo wa afya Tanzania, kwa kubuni mbinu mbalimbali za namna ya kuendesha mfumo wa afya nchini…tumeshirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma kwa muda mrefu kutoa mafunzo kwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni eneo la majaribio ya mafunzo haya na tumeona yakileta mabadiliko katika utendaji na uratibu wa shughuli za afya ya jamii na afya kinga kwa Mkoa wa Dodoma,”amesema.

Ameshukuru serikali baada ya miaka nane iliona afua hizo za msingi na zinaleta tija katika mfumo wa afya nchini na kuruhusu kutekelezwa nchi nzima.

“Ukiacha suala la Health Promotion pia tumesaidia katika CHF iliyoboreshwa ambayo mikoa yote Tanzania bara inatekeleza CHF iliyoboreshwa ambayo ni matunda ya mradi huu na fursa iliyopewa na serikali kubuni katika bima ya afya ya jamii, pia mfumo wa ugavi wa dawa tumekuwa tukisaidia namna ya kuangalia dawa zitapatikanaje pale ambapo hazipo kwenye Bohari ya dawa ya Taifa, tukatengeneza mfumo wa jazia au Mshitiri inatekelezwa Tanzania bara na hivi karibuni tumepata maombi ya serikali ya Zanzibar waje wajifunze namna ya kuboresha mfumo wa afya ikiwamo CHF,”amesema.

Amesema kuna changamoto nyingi nchini na mzigo wa magonjwa unaongezeka kwenye magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na namna ya kufanyia kazi mzigo huo unaondelea kuongezeka.

“Serikali imeandaa sera na miongozo ambayo utekelezaji wake umekuwa na changamoto na tumekuwa hatupati matokeo makubwa katika kudhibiti, kuzuia magonjwa hayo na tumeona ni vyema kuja na mbinu mpya, ili jamii kuepukana na magonjwa haya,”amesema.

Kwa upande wake, Mmoja wa washiriki ambaye ni Mratibu wa Elimu ya Afya katika Shule za Mkoa wa Dar es salaam, Dk.Ndeniria Swai, ameshukuru kupewa mafunzo hayo ambayo yamesaidia kuwapa uwezo mkubwa wa kutoa elimu ya afya kwa jamii. Amesema mafunzo hayo yamewajengea hali mpya ya kushirikiana kutoa elimu na yameonesha mapungufu ya mashirikiano yaliyokuwepo kwenye vitengo hivyo.

“Tumejifunza wanafunzi ni wananchi, na wananchi wanahaki ya kupata huduma ya afya na elimu na zinapaswa kwenda sambamba na hatutakuwa na mafanikio makubwa kama wahudumu hawa watajitenga katika utoaji huduma,”amesema.

Post a Comment

0 Comments