Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWAPA KAZI LUKUVI NA PROF. KABUDI,AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU CHAMWINO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Nape Moses Mnauye (Mb) kuwa Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari leo tarehe 10 Januari, 2022 katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb) kuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Hamad Yussuf Masauni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi leo tarehe 10 Januari, 2022 katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Hussein Mohamed Bashe (Mb) kuwa Waziri Kilimo leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Paschal Katambi Patrobass (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Pindi Hazara Chana (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Khamis Hamza Khamis (Mb) kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Ummy Hamis Nderiananga (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Prof. Eliamani Mathew Sedoyeka kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu Juma Selemani Mkomi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

...............................................

Na.Alex Sonna,Ikulu Chamwino

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametaja sababu za kuwaacha katika baraza lake la mawaziri aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabuni na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi huku akisema lengo lake ni kuwatumia kuwasimamia wengine.

Hivi karibuni Rais Samia alifanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri na Manaibu Mawaziri kwa kutowateua Lukuvi na Prof Kabudi hatua ambayo ilizua minongono kwa baadhi ya watu.

Akizungumza leo Januari 10,2022,mara baada ya kuwaapisha Mawaziri,Manaibu Mawaziri,Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu Ikulu Chamwino Jijini Dodoma,Rais Samia amesema akiwatizama Lukuvi na Kabudi ni kama Kaka zake hivyo kutokana na uzoefu wao katika kazi hatowaweka pembeni.

“Nina Kaka zangu wawili Lukuvi (William) na Kabudi (Paramagamba) nikiwatizama hawa age yao kama yangu na ukitizama niliowateua hamfanani kabisa kwahiyo kaka zangu wawili hawa nimewavuta waje kwangu waje wanisimamie.

Amesema Kabudi amefanya kazi nzuri kusimamia mazungumzo ya Serikali katika mikataba hivyo amemkabidhi rasmi kazi hiyo licha ya kwamba haipo katika mfumo.

Amesema Mashirika yote kazi zake ambazo zitaingia ubia na Serikali Kabudi ataongoza yote na yeye ndio Baba wa mikataba

“Kaka yangu Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia mazungumzo ya Serikali na mashirika na ndiyo kazi ambayo sasa nataka kumkabidhi kindaki ndaki aendelee na kazi hiyo ila kazi yake kwa sababu haipo katika muundo haitangazwi wala nini na yeye ndio atasimamia kazi hiyo.

Kuhusu Lukuvi amesema atakuwa na kazi nae hivi karibuni na huku akiwataka watu kupuuza maneno maneno yanayoendelea ya kwamba atagombea uspika.

“Kaka yangu Lukuvi yeye atakuwa na kazi na mimi mtaisikia baadae lakini namvuta Ikulu kazi yake ni kutusisimamia kwa sababu nikiwatizama hapo wote wanakaribia kustaafu miaka 2 wengine bado mna safari ndefu sasa ni kushika kiboko kuwasimamia nyie na Makatibu wakuu kwahiyo nimeona message afadhali Lukuvi katoka hajatoka yupo.

“Wengine wameanza kumletea message za ajabu ajabu wakijua atagombea uspika,hatagombania anakazi na mimi kwahiyo hatakuwa Spika wala hatagombania kwahiyo msianze kumchafua ametumikia Taifa hili kwa uadilifu kwa muda mrefu mwache aende na mimi amalize kazi,”amesema.

Kwa upande wake,Waziri mkuu Kassim Majaliwa, amesema kuwa atakaa pamoja na waziri walichaguliwa kupeana majukumu mbalimbali pamoja na kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Rais.

“Mheshimiwa Rais mara kadhaa umekuwa ukisisitiza kufanya kazi kwa matokeo chanya naomba nirudie kukuhakikishia kwamba kwenye mipango yetu na majukumu yetu tutahakikisha tunafanya kazi kwa matokeo chanja kuwatumikia wananchi na tunajua jukumu letu la kwenda kuwakuta wananchi mpaka kijijini kwenda kuwasikiliza wananchi kule walipo na changamoto na kuwahudumia jukumu hilo tutalitekeleza,”amesema.

Naye Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema kuwa bunge lipo tayari kushirikina na kuyafanyia kazi mambo yote yatakayoletwa na mkuu huyo wa nchi.

“Natoa ushauri kwenu kuwa Mhe. Rais Samia amewaamini kumsaidia, hizo kazi ni kazi zake hivyo ninyi mnapoenda kuzifanya kazi hizo fanyeni kama wasaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si vinginevyo.

“Kila mmoja ambaye ameteuliwa katika nafasi yoyote aliyoipata, Mhe. Rais Samia alishafanya kazi katika maeneo hayo kwa kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali, ninawapongeza kwa sababu mnayo sehemu ya kuanzia katika kuelezea mazuri ya Serikali hii,”amesema.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema Mahakama Kuu ya Tanzania itaendelea kushirikiana na wizara zote hasa wizara inayohusiana na teknolojia iweze kwenda kwa kasi, isiwe na vizuizi wala masharti mengi ili kuweza kukuza uchumi kwa kutumia TEHAMA. “Nawapongeza kwa imani ambayo mmepata kutoka kwa Mhe. Rais Samia ya kuweza kuchangia katika kustawisha maendeleo ya wananchi, muendelee kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Katiba na kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa na usalama.

“Hii ni karne ya 21 inayoongozwa na mapinduzi ya nne ya viwanda, sisi sote lazima tuchangie katika mapinduzi hayo, tunatakiwa kufanya kazi zetu kwa kutumia teknolojia kwa kasi zaidi ili ustawi wa wananchi tunaoutafuta upatikane kwa haraka zaidi,”amesema.

Post a Comment

0 Comments