Ticker

6/recent/ticker-posts

STEPHEN MASELE ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE


**********************

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa zamani wa Shinyanga na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mheshimiwa Stephen Julius Masele, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Masele anawania nafasi iliyoachwa wazi na Spika wa zamani wa Bunge hilo, Mheheshimiwa Job Ndugai aliyejiuzulu wiki iliyopita, huku Mbunge huyo aliyewahi pia kuwa Naibu waziri wa Nishati na Madini, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu ya January 10/2022 katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchukua fomu hiyo, Masele alisema kuwa ameamua kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya Spika, akitumia haki yake ya msingi ya Kikatiba, akiamini anao uwezo mzuri wa kuitumikia nafasi hiyo.

“Kwa sasa sina kubwa la kusema kwakuwa sio wakati sahihi kuzungumzia vipaumbele, ila ninachoweza kusema ni kuwa naweza kuisaidia serikali na Taifa endapo nitafanikiwa kuipata nafasi ya Spikan na kutoa mchango mkubwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za chama chetu cha CCM.

“Ni mapema mno kusema mengi ninayotaka kuyafanya, lakini naamini kwa kuzingatia Katiba na kanuni za Bunge kila kitu kitakwenda sawa, ambapo imeruhusu kila Mtanzania, hususan mimi ambaye ni mwanachama halisi wa Chama Cha Mapinduzi kujitokeza kuiwania nafasi hii,,” Alisema Masele.

Mbali na nafasi ya Spika wa Bunge kugombewa na wabunge, Chama Cha Mapinduzi kimeweka utaratibu mzuri wa makada wake kuchukua fomu ili kupendekezwa kuwania nafasi hiyo ambayo watu wa mwisho kupiga kura ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya taratibu zote ndani ya chama hicho kukamilika.

Post a Comment

0 Comments