Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AZIDI KUKIPAISHA KISWAHILI DUNIANI


**************************

Na John Mapepele

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan amesema Sera mpya ya mambo ya nje itaendelea kuzingatia pamoja na mambo mengine kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasia.

Mhe. Rais amesema hayo wakati akizungumza na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao Januari 24, 2022 hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe za mwaka mpya 2022 ( Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewashukuru wote waliopitisha maazimio ya kuifanya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya lugha ya Kiswahili duniani.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itahakikisha inasimamia maendeleo ya Lugha ya Kiswahili kwa faida ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu amefafanua kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha kubwa duniani ambayo vyuo vikuu, vyombo vya habari na wananchi wa nchi mbalimbali duniani wamekuwa wakitumia katika mawasiliano.

"Lugha ya Kiswahili ni kitu ambacho kitaliletea uchumi mkubwa taifa letu, tumejipanga kuliletea mapato makubwa taifa letu kupitia lugha hii” amesisitiza Yakubu

Ameongeza kuwa kupitia BAKITA mapinduzi makubwa yanakwenda kufanyika ikiwa ni pamoja na kubidhaisha lugha hiyo duniani.“

Post a Comment

0 Comments