
Waziri wa Utamaduni. sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa (katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul (wa kwanza kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Mhe.Said Yakubu wakifuatilia buruduni katika uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.












(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Utamaduni. sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaongoza wadau wa sanaa wa musiki nchini katika uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mchengerwa amesema katika uongozi wake hatotarajia kuona kuna watu wapo kwaajili ya kudhoofisha tasnia ya muziki nchini kwa kuwakandamiza wasanii.
Amesema kuna umuhimu nasi tukaandaa tuzo kubwa za barani Afrika kama MTV na AFRIMA hivyo amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha wanaandaa mazingira mazuri kwa kujifunza kwa nchi zingiine ambazo huandaa tuzo hizo.
"Sanaa ya muziki inanafasi muhimu sana,muziki uppo katika asili ya mwanadamu pia taifa linaweza kueleza hisia zake kwa kutumia muziki". Amesema Waziri Mchengerwa.
Katika zoezi la ugawaji wa mirabaha kwa wasanii, kwaya zimeonekana kupigwa na kusikilizwa zaidi katika vituo vya radio na luninga nchini nahivyo kuwafanya waimbaji wa nyimbo za injiri kuibuka na kitita zaidi katika mgao wa mrahaba wa kwanza ulianza kutolewa na Serikali kupitia Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA).
Kwaya Kuu ya Mtakatifu Cecilia Arusha imeibuka na mkwanja mzito wa Sh milioni 8.739 ikifuatiwa na Ali Saleh Kiba maarufu King Kiba aliyepokea Sh milioni 7.588 kutokana na mauzo ya nyimbo zake mbalimbali.
Wengine waliopokea mgao mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa ni Rose Mhando Sh. milioni 5.79.
0 Comments