Ticker

6/recent/ticker-posts

KAGERE AZIDI KUWA MTAMU, AIWEZESHA TIMU YAKE KUONDOKA NA ALAMA TATU DHIDI YA TANZANIA PRISON

***************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU y Simba Sc imefanikiwa kuondoka na alama tatu kwenye mchezo wa ligi ya NBC mara baada ya kuichapa Tanzania Prison bao 1-0 mchezo ulipigwa katika dimba la Benjamini MKAPA Jijini Dar es Salaam.

Tanzania Prison walianza mchezo kwa kipindi cha kwanza wakionekana kulinda sana lango lao na kushambulia kwa kushtukiza na kufanya ubao usomeke 0-0 kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba Sc iliendelea kulisakama lango la Tanzania Prison licha ya kukosa nafasi nyingi za wazi wakapata Penati dakika 67 ya mchezo, penati ambayo ilikuwa na lawama nyingi kwa wachezaji wa Tanzania Prison na refa.

Meddie Kagere alikwenda kupiga penati ambayo ilizaa bao la kuongoza na la ushindi kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake.

Post a Comment

0 Comments