Ticker

6/recent/ticker-posts

TRC WASAINI MKATABA WA UTENGENEZAJI MABEHEWA 1430 YA MIZIGO.



**************************

NA Emmanuel Kawau.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa amelitaka Shirika la Reli Nchini (TRC) kuhakikisha inasimamia kwa kikamilifu utengenezaji wa Mabehewa ya Treni ya kisasa (SGR) ambayo yatatengenezwa na Kampuni kutoka China inayofahamika kama CRRC inaternational na kukidhi mahitaji na matarajio ya watanzania.

Prof Mbarawa ameyasema hayo leo February 8,2022 Jijini Dar es salaam katika Zoezi la utiaji Saini Mkataba wa Ununuzi wa Mabehewa hayo kati ya Shirika la Reli Tanzania na Kampuni ya CRRC yatakayo gharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 127.2 sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya Shilingi bilion 300.

Aidha amesema utengenezaji wa mabehewa hayo unapaswa kukamilika katika muda uliopangwa kwa mujibu wa Mkataba ,nakwamba Bodi ya Wakurugenzi pamoja na timu itakayoenda nchini China kukagua utengenezaji huo inapaswa kuhakikisha mabehewa hayo yanakua na ubora unaotakiwa.

" Huu mradi unatakiwa ukamilike kwa muda uliopangwa naomba nitoe maagizo kwenu Bodi ya Wakurugenzi wa TRC na timu ya watu mtakaoenda china kuangalia utengenezaji wa mabehewa haya kuhakikisha mnafanya kazi hiyo kwa uzalendo,mabehewa yawe na kiwango cha ubora unaotakiwa,pia msikubali eksichuzi zozote tunataka mradi huu ukamilike kwa haraka ili ujenzi wa reli unapokamilika mabehewa yawe tayari"amesema Waziri Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TRC Masanja Kadogosa amesema mabehewa 1430 yatasaidia kubeba mizigo ya aina mbalimbali ikiwemo Mifugo,Mizigo ya jumla,Magari,Makontena,pamoja na Mafuta ambapo amesema kwamba mradi huo wa SGR utasaidia kukuza maendeleo ya Uchumi kwa Taifa la Tanzania pamoja na Nchi zingine kama vile Burudi,Rwanda.

"Behewa 600 kwaajili ya kubeba makasha,behewa 400 kwajili ya kubeba mizigo ya jumla ikiwemo sukari,chumvi,saruji,tumbaku,pamba na kahawa,behewa 190 kwaajili ya kubeba mafuta aina zote,behewa 70 kwaahili ya kubeba mabomba,mbao,magogo na vyuma,behewa 50 kwaajili ya kubeba magari na behewa 50 kwaajili ya kubeba wanyama" Alisema kadogosa.

Mwenyekiti wa bodi TRC Prof. John kondoro amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho wa wazi kuwa TRC inatekeleza maelekezo ya Mh rais ya kuhakikisha kuwa reli inajengwa kwa wakati na watu wapate huduma wanayoitegemea.

Nae Meneja Mkuu Msaidizi wa Kampuni ya CRRC International Tang Yun Peng ameihakikishia TRC kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia makubaliano yakimkataba yaliyosainiwa huku akiipongeza Tanzania kuwa endapo mradi wa SGR utakapokamilika utafungua milango yakiuchumi kwa nchi zingine za africa Mashariki na kati.

Post a Comment

0 Comments