Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA BALEHE WAPO HATARINI KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini Tacaids, Bw.Laiser Nyangusi akiwasilisha Mada wakati wa Semina ya Waandishi wa habari kuhusu hali ya Maambukizi kwa kundi la vijana nchini iliyofanyika mkoani Morogoro. Waandishi wa Habari wakifuatilia Semina iliyoandaliwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) mkoani Morogoro.

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, MOROGORO

Inakadiriwa kundi la vijana balehe lipo hatarini kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutokana na wengi wao wamekuwa hawana uelewa kuhusu UKIMWI hivyo kupelekea kuingia kwenye vishawishi na mwisho kupata maambukizi.

Ameyasema hayo leo mkoani Morogoro Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini Tacaids, Bw.Laiser Nyangusi wakati wa Semina ya Waandishi wa habari kuhusu hali ya Maambukizi kwa kundi la vijana nchini.

"kundi ambalo lipo hatarini kupatwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni kundi la Vijana kuanzia miaka 15 hadi 24 ambapo kundi hilo limekumbwa na ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu gonjwa hili hatari la UKIMWI". Amesema

Amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2016/2017 takwimu zinaonesha asilimia 84% wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wanajitambua hali zao, kati ya hao asilimia 98% wako kwenye dawa na asilimia 92% wamefubaza virusi.

Post a Comment

0 Comments