Ticker

6/recent/ticker-posts

WCF BONANZA LAFANA

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma ametoa wito kwa watumishi wa Mfuko kujijengea utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya kuimarisha afya zao.

Rai hiyo imetolewa wakati wa Bonanza la WCF lililofanyika tarehe 05/02/2022 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo watumishi wa Mfuko walishiriki.

"Michezo ina manufaa makubwa kwa afya zetu hasa katika nyakati hizi za magonjwa yasiyoambukiza hivyo tuzingatie mazoezi ili yatuweke katika hali nzuri kimwili na kiakili", alisema Dkt. Mduma.

"Michezo pia inaboresha mahusiano yetu kama watumishi pamoja na majirani zetu na wananchi kwa ujumla hivyo tuendeleze utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara", aliongeza Dkt. Mduma.

Michezo mbalimbali ilihusika kwenye bonanza hilo la WCF ikiwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba, jogging, riadha, kukimbiza kuku pamoja na kukimbia ndani ya magunia ambapo washindi walitunukiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na medali.





























Post a Comment

0 Comments