Ticker

6/recent/ticker-posts

"BARAZA LA WAFANYAKAZI KUWENI WAWAZI NA KUKOSOA MAPUNGUFU"-WAZIRI SIMBACHAWENE

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geogre Simbachawene akizungumza na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo mara baada ya kufungua mkutano wa baraza leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe. Mary Makondo akizungumza mara baada ya ufunguzi mkutano wa baraza hilo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika ufunguzi wa mkutano wa baraza hilo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geogre Simbachawene akipata picha ya pamoja na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria mara baada ya kufungua mkutano wa baraza hilo leo tarehe 10/03/2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Baraza la wafanyakazi wa wizara ya katiba na sheria limetakiwa kuwa wazi,kutoa mapendekezo, na kukosoa mahala ambapo kuna Mapungufu ya kiutendaji ili kuweza kuboresha wizara hiyo katika utendaji wa kazi.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 10,2022 Wakati akifungua mkutano wa baraza hilo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geogre Simbachawene amesema kuwa ni vema wafanyakazi wakawa wazi Kuzungumza kama kuna mapungufu mahali ili wizara iweze kuboresha zaidi.

"Mnaposikia jambo lolote lazima mlifanyie kazi, mkisifiwa mjue kazi mnayoifanya iko vizuri lakini mkisikia mmesemwa vibaya mjitafakari mjue wapi mnakosea ili muweze kujirekebisha na mambo mengine yaende". Amesema

Aidha Waziri Simbachawene amewataka wafanyakazi hao kutimiza majukumu yao ya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha wizara hiyo inasonga mbele kwa kuwa na umoja wa kazi katika kuwaletea maslahi watanzania.

Katika hatua nyingine Simbachawene amesema kuwa ni vema kubadilisha mfumo wa upimaji wa watumishi wa umma kwa kufanya utafiti ili kuongeza ufanisi wa kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni katibu mkuu wa wa Wizara hiyo Mhe. Mary Makondo ameahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri na kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kuweza kutimiza malengo yaliyopo kwenye bajeti ya Wizara hiyo.

Post a Comment

0 Comments