Ticker

6/recent/ticker-posts

CHAUREMBO- HONGERA RAIS SAMIA SULUHU KWA KUTAFUTA FEDHA ZINAZOWEZESHA KUTEKELEZA MIRADI YA TASAF NCHINI


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Wikichi wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Njombe.

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Wikichi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Njombe.


Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakiongozana na Wananchi wa Kijiji cha Wikichi kutazama Mradi wa ujenzi wa zahanati ya Wikichi wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Njombe.


Sehemu ya mwonekano wa jengo la Zahanati ya Wikichi iliyofadhiliwa na TASAF pamoja na Michango ya Jamii. Zahanati hiyo imetembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Njombe.

*************************

Na. Veronica Mwafisi-Njombe

Tarehe 19 Februari, 2022

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI), Mhe. Abdallah Chaurembo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutafuta fedha kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Mhe. Chaurembo amesema hayo alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Njombe.

Mhe. Chaurembo amesema, Kamati yake inamshukuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha ambazo zimetekeleza Mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Wikichi ambao umesogeza karibu huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.

Mhe. Chaurembo ameongeza kuwa, Kamati yake imepokea taarifa kutoka kwa Mratibu wa TASAF wa eneo hilo pamoja na kukagua zahanati hiyo iliyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 89 iliyojumuisha na vifaa tiba, hivyo imeridhika kutokana na kazi nzuri iliyofanyika.

Vilevile, Mhe. Chaurembo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Ladislaus Mwamanga kwa kupeleka wataalam ambao wamesimia vizuri ujenzi wa zahanati hiyo.

Mhe. Chaurembo amempongeza pia mratibu wa TASAF kwa kusimamia vema fedha zilizotolewa na Mhe Rais kujenga Zahanati hiyo ambayo imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani.

Sanjari na hilo, Mhe. Chaurembo amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Wikichi kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kuhakikisha ujenzi wa Zahanati hiyo unakamilika kwa wakati.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) inaendelea na ziara yake ya kikazi kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika Halmshauri ya Wilaya Mji Njombe.

Post a Comment

0 Comments