KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben kabla ya kuanza kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakiedelea kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakimsikiliza Mkandarasi Johannes Nyamasiriri wakati wakikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben wakati wakikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakikagua kisima cha maji kinatumia na wananchi waliopo karibu na Pori la Akiba Swagaswaga wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Ally Makoa,akiipogeza TAWA kwa usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha mara baada ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Shaban Shekilindi akizungumza mara baada ya kukagua na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
MKURUGENZI wa Idara ya Wanyamapori Dk.Maurus Msuha,akiipongeza Kamati hiyo kwa kutembelea na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali katika Pori la Akiba Swagaswaga lililopo wilaya za Chemba na Kondoa.
KAIMU Kamishna wa Uhifadhi katika Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Nyanda,akieleza majukumu yanayotekelezwa na TAWA wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii ya kukagua na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben,akitoa taarifa ya utedaji kazi ya Pori la Akiba Swagaswaga kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii ilipofanya ziara ya kukagua na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
KAMANDA wa Uhifadhi Pori la Akiba Mkungunero Khadija Malongo,akiiomba kamati hiyo iweze kutembelea Pori la Mkungunero wakati wa ziara ya kukagua na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
SEHEMU ya watumishi wa TAWA,Waandishi na waheshimiwa wabunge wakifatilia hotuba mbalimbali.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TAWA mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.
................................................
Na Alex Sonna-KONDOA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miradi ya maendeleo katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa .
Miradi ambayo imekaguliwa na kamati hiyo ni Ujenzi wa Ofisi, ujenzi wa nyumba za watumishi, kisima kinachotumia pampu za kisasa pamoja na ujenzi wa nyumba za kulala wageni 'Hostel' yote ikigharimu kiasi cha shilingi billioni 1.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Ally Makoa amesema wameridhishwa na matumizi ya fedha zilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza miradi hiyo.
“Tunamshukuru Rais kwa kuleta fedha nyingi katika Wizara za Ardhi na ile ya Maliasili na Utalii naipongeza Wizara ya Maliasili kwa kuzisimamia vizuri fedha hizo.Niwatakie kila la heri na mwambie Waziri (Dkt Damas Ndumbaro) Kamati imeridhishwa na kazi na tukiingia katika bajeti tutaendelea kumshawishi mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) aongeze fedha,”amesema.
Aidha,Makoa ambaye ni Mbunge wa Kondoa Mjini amesema kuna maeneo machache katika Mkoa wa Dodoma ambayo yakiwekezwa nguvu yanaweza kunyayuka kiutalii likiwemo pori la Swagaswaga na Mkungunero.
Vilevile,Mwenyekiti huyo ameitaka Wizara hiyo kusimamia fedha ambazo zinatolewa na Rais Samia ili awe na imani na kuweza kuongeza fungu lingine.
“Tukifanya vizuri ndio atatuletea fedha zaidi lakini kama kutakuwa na ‘mazongezonge’ kwenye fedha anazoleta wakati mwingine hataongeza tunatarajia fedha yoyote itakayoletwa itatumika kisawasawa,”amesema.
Aidha ameipongeza TAWA kwa kuwa na mahusiano mazuri na jamii ambazo zipo pembezoni mwa mapori ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za maji katika vijiji.
Kwa upande wake,Kaimu Kamishna wa Uhifadhi kutoka TAWA,Mabula Nyanda Amesema utekelezaji wa mradi huo utasaidia Mamlaka kutimiza lengo la kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii kama ilivyoanishwa katika ilani ya CCM.
“Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kutatua migogoro kati ya hifadhi na wananchi ambayo imesaidia kuboresha mahusiano baina ya pande hizi mbili,”amesema.
Naye,Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben amesema katika kuhakikisha migogoro kati ya wananchi na wahifadhi inapungua wameendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi.
Amesema kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Desemba 2021 wamefanikiwa kuelimisha jumla ya wananchi 4604 katika vijiji 18 ambapo amedai elimu hiyo imetolewa kwa kushirikiana na Afisa Wanyamapori na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa Wilaya za Chemba na Kondoa.
0 Comments