Ticker

6/recent/ticker-posts

TUZO ZA MALKIA WA NGUVU 2022 ZATOA HAMASA KWENYE JAMII

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akipokea tuzo ya Malkia wa nguvu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Bw.Joseph Kussaga katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifurahi jambo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Mhe..Joseph Kussaga katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James wakifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Mhe.Joseph Kussaga akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wetu wa Maendeleo ya Biashara Clouds Media Group , Bi.Sheba Kussaga akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe.Kitila Mkumbo akifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Goba Mushroom Zone wakabidhiwa Tuzo ya Malkia wa Nguvu kipengele cha Saiti ya Kilimo Biashara katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.Mwanzilishi wa kampuni ya Katty Collection akipokea tuzo ya Malkia wa nguvu 2022 kipengele cha Saiti ya Mitindo na Urembo katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Mchambuzi wa michezo Bi.Jesca Kishamba akikabidhiwa jukumu la kupokea tuzo ya Malkia wa Nguvu 2022 Saiti ya Michezo kwa niaba ya Timu ya Taifa ya Twiga Stars katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Chief Jaji wa mashindano ya BSS Madam Rita Paulsen akikabidhiwa tuzo ya Malkia wa Nguvu kipengele cha Saiti ya Burudani kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wakifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Msanii wa Kizazi kipya Bongo fleva Juma Jux akitumbuiza katika hafla ya utoaji tuzo kwa Malkia wa Nguvu 2022 iliyofanyika Usiku wa kuamkia terehe 27/03/2022 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI imeipongeza Clouds Media Group kwa kuendesha programu ya Malkia wa nguvu yenye kauli mbiu "Tupo Site" na kuwapa moyo wale wanawake wajasirimali wanaoenesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali kwenye jamii.

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo za Malkia wa Nguvu zilizotolewa usiku wa kumkia tarehe 27/03/2022, Mlimani City Jijini Dar es Salaam Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema Clouds imekuwa ikiiunga mkono serikali kwa muda mrefu hivyo wattendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kutokana na mchango mkubwa ambao wamekuwa wakitoa kwenye jamii.

Waziri Gwajima amesema hapa nchini wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wetu ambapo kitaifa asilimia themanini (80%) ya nguvu kazi ya Sekta ya kilimo ni wanawake na wanawake hawa huzalisha asilimia sitini (60%) ya chakula chote hapa nchini.

"Katika baadhi ya familia, wanawake ndio wahimili wakuu kwa maana ya upatikanaji wa chakula, mavazi na huduma nyingine za kijamii zikiwemo za kuwapeleka watoto shule na za afya kwa maana ya kuwahudumia wanafamilia ambao ni wagonjwa". Amesema Waziri Gwajima.

Amesema pamoja na mchango mkubwa wa wanawake kwenye maendeleo ya jamii, nchini Tanzania na katika nchi nyingine duniani wanawake wanaendelea kukabiliana na changamoto ya kuwa na uchumi duni ikilinganishwa na wanaume jambo ambalo siyo haki.

Aidha amesema Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 62.68 katika mwaka wa fedha 2020/21 kwa ajili ya Mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika halmashauri zote nchini ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2021 jumla ya Shilingi bilioni 53.81 zilikopeshwa kwa Vikundi 7,993 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu sawa na 86%. Kati ya fedha hizo shilingi Bil. 28.17 zilitolewa kwa vikundi vya wanawake 4,894 vilivyozalisha ajira 52,428.

Pamoja na hayo Waziri Gwajima amesema Serikali inampango wa kuondoa kero kwa wajasiriamali wakiwemo Wajane, lishe na wauza mbogamboga kwa kupatiwa maeneo rasmi ya kufanyia biashara yenye ukubwa wa hekta 15,822.64 katika Halmashauri 150 nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa (Sensa) kwani ni muhimu kwa kupata takwimu sahihi za watu na makazi ili kuwezesha Serikali kufanya makisio na kupanga mapato na matumizi katika shughuli za serikali.

"Wanawake ni kundi ambalo tunatakiwa kuwa mbele kuitikia zoezi la sensa mwaka huu wa 2022 na tuwaelimishe na wenzetu ili nao waweze kushiriki zoezi hili ambalo ni muhimu kwa taifa kwa ujumla". Amesema

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Mhe..Joseph Kussaga amewapongeza watumishi wote wa Clouds Media Group kuhakikisha inawapa kipaumbele wanawake kwenye kazi na kufanya tamasha hilo kuwa kubwa na lakihistoria hapa nchini.

"Zamani mimi na Ruge tulikuwa hatuwezi kulala tukamuachie mtu kazi, ila Leo nalala kabisaaaa, nakuja kwenye Shughuli nakuta show imesimama vizuri". Mhe.Kussaga

Post a Comment

0 Comments