Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA SUKARI YA KILOMBERO YAWASIHI WAFANYABIASHARA KUTOPANDISHA BEI YA SUKARI HOLELA KATIKA MFUNGO WA RAMADHANI***********************


Na Magrethy Katengu, Dar es salaam


Ikiwa imesalia siku kadhaa kuanza mfungo wa ramadhani mwenzi Mtukufu Kampuni ya Sukari Kilombero imewasihi Wafanyabiashara wote wa jumla na rejareja wanaouza bidhaa za "Bwana Sukari kutokupandisha bei katika kipindi hicho ambapo mfungo wa ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzo mwa mwezi aprili mwaka huu ili kusaidia kuepuka taharuki inayoweza kujitokeza kwenye kipindi Cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa ramadhani.


Tamko hilo ametolewa leo Jijini Dar es salaam Mkuu wa idara ya biashara wa kampuni ya Sukari kilombero Bw.Fimbo Butallah wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema kutokana na historia yakupanda kwa bei ya bidhaa za vyakula kila uanzapo mfungo wa mwezi Mtukufu wa ramadhani nakusababisha adha kubwa kwa waumini wanaofunga mwezi huo.


Hata hivyo Butallah amesema katika uchumi wa soko huria wao Kama wazalishaji hawaruhusiwi kuwapangia Wafanyabiashara bei yakuuza bidhaa lakini wanawajibu mkubwa wakuwashauri upandishaji holela wa bei hasa pale ambapo wazalishaji hawajapandisha bei ya bidhaa hiyo.


" Tunawasihi Wafanyabiashara kote Nchini kutopandisha bei ya Sukari katika Mwezi Mtukufu wa ramadhani ili kuepuka taharuki inayoweza kujitokeza " amesema kuu huyo wa idara ya biashara wa kampuni ya Sukari Kilombero.


Sanjari na hayo Bw.Butallah ameongeza kwa kusema kuwa suala la uhaba wa Sukari ambalo Mara nyingi limekuwa likijitokeza kwenye mfungo wa ramadhani Kampuni ya Sukari Kilombero inayo akiba yakutosha kulivusha Taifa katika mfungo huo Mtukufu nakuongezea ,ambapo tayari kampuni imepata kibali chakuagiza Sukari kutoka nje ya Nchi kuziba pengo la uzalishaji.


" Tumekwisha anza taratibu za uagizaji wa Sukari ambayo inatarajiwa kuanza kuingia nchini muda wowote kuanzaia hivi Sasa tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuhusu upandaji holela wa bei ya Sukari hususani chapa ya " Bwana Sukari" kwani kampuni imeandaa mikakati thabiti kukabiliana na tatizo hilo katika msimu huu" amesema Butallah.


Aidha Kampuni ya Sukari ya Kilombero ambayo inamilikiwa na Kampuni ya An illovo Sugar Africa kwa asilimia 75 na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 25, ipo katika maandalizi ya Mradi wake wa upanuzi ambao utakuza uwezo wa kampuni hiyo wa kuzalisha Sukari na kupunguza uhaba wa Sukari Nchini kupitia chapa yake ya "Bwana Sukari"

Post a Comment

0 Comments