Ticker

6/recent/ticker-posts

MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA RAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA WIKI YA WAZAZI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa Amani Unguja kuhudhuria ufunguzi wa Kongamano la Jumuiya ya Wazazi Tanzania.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Tuzo Maalum iliyotolewa na Jumuiya ya Wazazi Tanzania akikabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Wazazi Tanzania Bw. Haidar A.Haji , wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Wazazi Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa Amani na (kulia kwa Rais) Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)

WAHESHIMIWA Wabunge,Wawakilishi na Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wakifuatilia hutuba ya Ufunguzi wa Kongamano la kuadhimisha Wiki ya Wazazi Tanzania, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia na kulifungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa Amani Unguja leo.26-3-2022.(Picha na Ikulu) MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Tuzo Maalum ya kuthamini Mchango wake kwa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, akikabiwa na Makamu Mwenyekiti wa Wazazi Bw.Haidar A.Haji na (kushoto kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mwenyekiti wa Wazazi Tanzania Bw.Edmond Mndolwa, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Wazazi Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa Amani Unguja leo 26-3-2022.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM.Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Viongozi wa meza kuu (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Bw.Edmond Mndolwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr.Abdalla Juma Mabodi, wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa Amani Unguja.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments