Ticker

6/recent/ticker-posts

TaSUBa YAHIMIZWA KUJIKITA ZAIDI KWENYE UBUNIFU

Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mwambao Bagamoyo, Bi.Dorice Mwakatobe akikabidhi vyeti kwa wahitimu wakiwa kwenye mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mfupi kwa wa Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mwambao Bagamoyo, Bi.Dorice Mwakatobe akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mfupi kwa wa Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mfupi kwa wa Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu Kusini Mwa Tanzania(STUM) Mch.Mark Walwa Marekana akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mfupi kwa wa Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Mmoja wa wahitimu akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi katika mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mfupi kwa wa Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mfupi kwa wa Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

************************

Wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mfupi kwa wa Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wametakiwa kufanya muziki ambao unamatokeo mazuri kwa maendeleo ya kanisa,kiriho na kijamii.

Wito huo umetolewa leo na Mgeni Rasmi kwenye mahafali TaSUBa, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mwambao Bagamoyo, Bi.Dorice Mwakatobe ambapo amesema licha ya wahitimu hao 58 kumaliza mafunzo hayo wanatakiwa kutumia mafunzo hayo kuleta matokeo chanya kwenye jamii.

Amewataka wahitimu kuwa mabalozi wazuri kule waendako ili wengine waweze kupata fursa kujiunga na TaSUBa na kuendeleza vipaji vyao.

Pamoja na hayo Bi.Dorice ameshauri Chuo kuendelea kuwa wabunifu wa kuanzisha kozi mbalimbali ambazo zitawavutia watu wengi na kuwa na soko kwa sekta binafsi na za Serikali.

"Nawapongeza TaSUBa kwa kazi nzuri ya kutoa mafunzo na viongozi wa kanisa kutoa malezi kwa wahitimu hawa wakati wote walipokuwa hapa chuoni". Amesema Bi.Dorice.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye amewapongeza viongozi wa kanisa la Waadventista Wasabato kuungana na taasisi hiyo kwa kutoa ushirikiano wa kutosha hasa katika masuala ya muziki wa injili na imani pindi mafunzo yakiwa yanaendelea.

Sanjali na hayo Dkt.Makoye amewataka wahitimu kuyafanyia kazi yale yote waliyojifunza ili waweze kuona faida ya hayo mafunzo.

"Wahitimu mkitoka hapa basi mkaoneshe hicho mlichokipata hapa waliobaki waone mabadiliko lakini pia muendelee kukifanyia kazi ili kiweze kukua na na hatimae kufikia lengo". Ameeleza.

Nae Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu Kusini Mwa Tanzania(STUM) Mch.Mark Walwa Marekana Amesema Kanisa la Waadventista Wasabato lipo na litaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na TaSUBa kwaajili ya kutengeneza kitu ambacho kitampendezesha mwenyezi mungu.

Pamoja na hayo ameiomba Taasisi ya TaSUBa kuhakikisha wanaendelea kuibua vipaji vya vijana wakitanzania na baadae nchi za jilani kutamani kujiunga na Chuo hicho cha Sanaa na kuweza kukitangaza Duniani kote.

Amesema kuna uwezekano mkubwa mmoja wa Botswana ataweza kujiunga na chuo hicho kwani taarifa hizo anazo hivyo TaSUBa watengeneze vopeperushi vya kutosha viweze kufika katika nchi hiyo ili nawengine waweze kujumuika na kujiunga na Taasisi hii". Amesema Mch.Marekana.

Vilevile kwa upande wake mmoja wa wahitimu akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi amesema , pamoja na mafunzo kufanyika TaSUBa wahusika walifanya mafunzo kwa vitendo kwenye makanisa yao yale waliofundishwa TaSUBa.

Amesema kushiriki katika mafunzo hayo wamepata mtazamo tofauti wa namna ya kuendesha ibada ya nyimbo makanisani pamoja na kutambua falsafa ya muziki wa kanisa la Waadventista Wasabato.

"Kila aliyehudhuria masomo haya ya muziki amefungua mlango wa kujifunza muziki kama vile utunzi, piano, mitambo, falsafa, uimbaji na uimbishaji". Amesema

Post a Comment

0 Comments