Ticker

6/recent/ticker-posts

TMA YATOA TAARIFA YA MWENENDO WA HALI YA KLIMATOLOJIA ILIVYOKUWA MWAKA 2021

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo kwa waandishi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Huduma za Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang'a.



*****************************



Na Mwandishi Wetu


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa rasmi ya Mwenendo wa Hali ya Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021, huku ikiainisha ulikuwa na hali mbaya ya kiujumla iliyoambatana na madhara kwa baadhi ya maeneo.


Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari leo jijini dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi alisema kwa mwaka 2021 Tanzania ilikumbwa na matukio ya hali mbaya ya hewa hususan mvua kubwa zilizoambatana na mafuriko na upungufu wa mvua pia katika baadhi ya maeneo, joto pamoja na upepo mkali.


"...Itakumbukwa kuwa mwaka wa 2021, nchi yetu ilikumbwa na matukio ya hali mbaya ya hewa hususan mvua kubwa zilizoambatana na mafurikona upungufu wa mvua katika baadhi ya maeneo, joto pamoja na upepo mkali. Maeneo yaliyoathiliwa na mafuriko ni pamoja na mikoa ya kusini na magharibi mwa nchi ambapo yalisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo barabara na madaraja, makazi, na mashamba," alisema Dkt. Kijazi.


Alitolea mfano, kuwa tarehe 12 Januari 2021 Mvua kubwa ya milimita 369.7 ilinyesha Mtwara na kuvunja rekodi ya mvua iliyowahi kupimwa ndani ya saa 24 katika Kituo cha Hali ya Hewa cha Mtwara tangu kuanzishwa kwake mwaka 1951. Pia, mvua ya mawe iliyoleta taharuki ilinyesha wilayani Biharamulo tarehe 14 Agosti 2021, kipindi ambacho kawaida huwa hakina mvua kwa maeneo hayo.


Hata hivyo, aliongeza kuwa kipindi cha ukavu cha muda mrefu kilitokea katika miezi ya Oktoba na Disemba 2021 na kusababisha athari kubwa kwa jamii na uchumi hasa jamii za wafugaji ambapo idadi kubwa ya mifugo ilikufa kwa njaa na kukosa maji katika baadhi ya maeneo ya mikoaya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Manyara na Pwani.


"...Kutokana na changamoto hizi za hali ya hewa ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara, Mamlaka imejikita kufanya uchambuzi wa kina wa hali ya hewa kila mwaka na kisha kutoa ripoti ya hali ya Klimatolojia kwa mwaka husika," alisisitiza Dkt. Kijazi ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).




Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo kwa waandishi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Huduma za Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang'a.


Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Huduma za Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang'a akifanya wasilisho kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akisisitiza jambo alipokuwa akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo jijini Dar es Salaam.



Aidha, ripoti hiyo inatoa taarifa za kina kuhusu matukio ya hali mbaya ya hewa yaliyotokea na madhara yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia hubainisha ukubwa wa matukio haya kwa kulinganisha na matukio ya namna hiyo yaliyotokea miaka iliyopita. Mwaka 2021 ulikuwanajotojuuyawastaniwamudamrefu (1981-2010) kwa kiwango cha nyuzijoto0 50C. Hali kama hiyo inaweza ikawa imeathiri afya ya binadamu na wanyama, uzalishaji, usindikaji na uhifadhi wa vyakula.


"Sambamba na Taarifa hii ya Klimatolojia, napenda nitumie fursa hii tena kukumbusha hususan wataalam katika sekta mbalimbali kufuatilia taarifa mpya ya tathmini ya mabadiliko ya hali ya hewa kuhusiana naA thari na Uhimilivu wa mabadiliko ya hali ya hewa iliyotolewa la tarehe 28 Februari 2022 na Jopo la Kiserikali la Tathmini ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC)."

Post a Comment

0 Comments