Ticker

6/recent/ticker-posts

WATU 13 WAPOTEZA MAISHA, NA WENGINE 32 WAJERUJIWA KWENYE AJALI YA GARI MOROGORO************

WATU 13 wamefariki Dunia na wengine 32 kujeruhiwa baada ya basi lenye namba za usajili T 732 ATH mali ya Kampuni ya AHEED linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Tanga kugongana na lori lenye namba IT 2816.

Akizungumza Kwa njia ya simu na fullushangwe Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Futunatus Muslim amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Malela wilayani Mvomero mkoani hapa.

Amesema majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Post a Comment

0 Comments