Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA WAZIRI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI WA SAUDI ARABIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi na ujumbe wake hawapo pichani walipokutana katika ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kulia ) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia (hawapo pichani) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akifuatilia mazungumzo hayo katika kikao kilichofanyika jijini Riyadh
Ujumbe wa Saudi Arabia (kushoto) katika kikao cha pamoja na ujumbe wa Tanzania (kushoto) walipokutana katika Ofisi za Wizara ya Biashara na Uwekezaji jijini Riyadh
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa nne kutoka kushoto) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi na ujumbe wake hawapo pichani walipokutana katika kikao jijini Riyadh.
Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake akizungumza katika kikao na Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake hawako pichani walipomtembelea ofisini kwake jijini Riyadh
Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi akimpa zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.
Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabiakimpa zawadi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, akimpa zawadi Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.
Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi (aliyenyoosha mikono) akielezea jambo wakati akiwasindikiza Waziri Mulamula na ujumbe wake mara baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Riyadh nchini humo.

************************


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah Al- Qasabi katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri Mulamula amemuhakikishia Mhe. Dkt. Al-Qasabi utayari wa Tanzania katika kushirikiana na Saudi Arabia kuptia sekta za mifugo, uvuvi, uwekezaji na usafiri wa anga.

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Mkurugenzi wa Idara ya Mashriki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza, kaimu Mkurugenzi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bibi Anna Lyimo na wawakilishi wa wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima kutoka Tanzania Bara .

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini humo na wafanyabiashara marafiki wa Tanzania walioko jijini Riyadh.

Balozi Mulamula na ujumbe wake pia wanatarajia kukutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara walioko katika miji ya Jeddah na Makkah katika mkutano utakaofanyika jijini Jeddah.

Waziri Mulamula na ujumbe wake waliwasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi tarehe 9 ikiwa ni mualiko uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alipotembelea Tanzania mwezi Machi 2021. Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

Post a Comment

0 Comments