Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MWAKILISHI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI CZECH

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Jamhuri ya Czech katika sekta za biashara na uwekezaji, kilimo, elimu na teknolojia.

Balozi Mulamula aliwakaribisha wawekezaji kutoka Czech kuwekeza nchini pamoja na kutia mkazo wa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Czech.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech, Bw. Grolig amesema ataendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Czech kuja kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu salama ya kuwekeza.

“Jamhuri ya Czech imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania na katika kutimiza azma hiyo, wafanyabiashara na wawekezaji wameonesha nia ya kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza ndege ndogondogo Pamoja na magari makubwa hapa Tanzania,” amesema Bw. Grolig

Pia ameongeza kuwa kwa sasa Czech ipo katika mchakato wa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hapa nchini Tanzania ili kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi kuja Tanzania kutafuta fursa za uwekezaji,” amesema Bw. Grolig.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme na Afisa mambo ya Nje kutoka Wizarani, Bibi Kisa Mwaseba. Kushoto mwa Bw. Grolig ni maafisa alioambatana nao kutoka Jamhuri ya Czech


Post a Comment

0 Comments