Ticker

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE MMOJA MBARONI TUHUMA ZA MAUAJI YA MTOTO WA UMRI WA MIAKA MIWILI NA MIEZI NANE


****************

NA Magrethy Katengu- Dar es salaam

Mwanamke mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili na miezi minne.

Akizungumza leo na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi ASP Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina Latifa Bakari mwenye umri (33), mkazi wa Mabibo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi mnamo Aprili 05/mwaka huu mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi mtoto huyo baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa Aprili 6 mwaka aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu), kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side Ubungo.

Pia baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, Polisi wakafanya uchunguzi kwa kumuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa.

Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi limewakamata watu wanne (4) kwa tuhuma za kujaribu kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanesco ikiwemo Nyaya aina ya Copper kwa lengo la kuziuza watuhumiwa hao; ni Omary Ally miaka 28, Mchaga, mkazi wa Tegeta na mwezake Juma Suleimani , Miaka 30, Mrangi, mkazi wa Wazo na wanunuzi wa vifaa hivyo ni Amosi Johni, miaka 30, Msukuma, mkazi wa Tegeta na Molokole Machage miaka 26, Mkurya mkazi wa Bunju walikamatwa mnamo Aprili 10 mwaka huu watuhumiwa wote hawa wamehojiwa kwa kina na kukiri kuhusika katika matukio ya namna hiyo baada ya kupekuliwa maeneo yao walikutwa na viroba vinne vya Nyaya za Copper zilizochunwa

Aidha Jeshi la Polisi linaendelea kutoa onyo kali kuwa halitamvumilia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma na atakayejaribu atakamatwa na mifumo ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria itazingatiwa.

Post a Comment

0 Comments