Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS WA TAHLISO AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI ZOEZI LA SENSA


*************

RAIS wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Juu ( TAHLISO) Frank Nkinda, amewataka wananchi wakiwemo wanafunzi kujitokeza kwa wigi kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Nkinda alisema ni muhimu kwa kila mtanzania kushiriki kikamilifu katika mchakato huo kwa lengo la kusaidia ukuaji wa maendeleo ya nchi kama ambavyo Rais Samia amesisitiza.

" Sensa ni muhimu, hauwezi kupanga maendeleo ya nchi kama hujajua idadi ya watu ulionao, Rais amesisitiza kuwa sote ni vyema tukajitokeza na kushiriki katika zoezi hilo Agosti 23 Mwaka huu, niwasihi tusimwangushe, tujitokeza kikamilifu" alisema Nkinda

Alisema kama Taifa kuna manufaa mengi ya kushiriki sensa hiyo, hivyo ni vyema kila mtu akaona umuhimu wake na kujitokeza siku hiyo kufanikisha suala hilo litakalotusaidia watanzania katika kujiletea maendeleo.

Aidha alisema amekusudia kufanya kongamano maalumu litakalowashirikisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadiliana juu ya umuhimu wa wananchi kushiriki zoezi hilo kwa lengo la kuchochea hamasa ya ushiriki wake.

Awali akizindua nembo ya sensa hiyo sambamba na tarehe ya kufanyika kwake, Rais Samia Suluhu Hassan alisesema zoezi hilo i muhimu kwa kuwa litaisaidia Serikali kuandaa sera na mipango mipya ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu na jinsi ya kuitekeleza na kufatilia utekelezaji wa mipango hiyo.

Alisema taarifa hizo zitakazopatikana kupitia zoezi hilo pia zitasaidia kujua wastani wa ongezeko la watu na hali ya uhamiaji mfano kutoka vijijini kuja mjini lakini hata waliotoka nje kuhamia na kuingia Tanzania.

"Sensa pia itatusaidia Serikali kufanya maamuzi kuhusu ugawaji wa rasilimali za Taifa na kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo afya, elimu, maji, umeme, ujenzi wa miundombinu kulingana na idadi ya watu na mahitaji ya maeneo hayo" alisema Rais Samia.

“Ili Sensa iweze kukidhi mahitaji ya kufanikisha malengo yote hayo ni lazima ishirikishe watu wote. Zoezi hili litakuwa ni kwa watu wote waliolala na kuamkia siku ya Sensa kwenye nchi ya Tanzania,” alisema Rais Samia.

Alisema licha ya uwepo wa tozo za makazi, Serikali haikuwa na idadi sahihi ya nyumba na makazi, hivyo zoezi hilo litatoa ubora kwa kujua anuani za makazi, idadi ya majumba na aina za nyumba zilizopo.

Post a Comment

0 Comments