Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM WAINGIA MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA ROCKET TANZANIA LIMITED KWENYE UTAFITI WA GESI YA HELIUM


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Prof. william Anangisye (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Rocket Tanzania Limited Bw. Justyn Wood wakisaini Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Prof. william Anangisye (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Rocket Tanzania Limited Bw. Justyn Wood wakionesha mikataba mara baada ya kusaini Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Prof. william Anangisye (kushoto) akipeana pongezi na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Rocket Tanzania Limited Bw. Justyn Wood wakati wa utiwaji saini wa Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022 Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza wakati wa utiwaji saini wa Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Prof. william Anangisye akizungumza wakati wa utiwaji saini wa Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022.Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Rocket Tanzania Limited Bw. Justyn Wood akizungumza wakati wa utiwaji saini wa Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022.Kaimu Amidi wa Shule Kuu ya Madini na Jiosayansi Dkt. Emmanuel Kazimoto akizungumza wakati wa utiwaji saini wa Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022. Meneja wa Kampuni ya Rocket Tanzania Limited Nchini Bw. Joseph Uiso akizungumza wakati wa utiwaji saini wa Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022. Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akiwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Prof. william Anangisye, Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Rocket Tanzania Limited Bw. Justyn Wood pamoja na wadau mbalimbali wakipata picha ya pamoja wakati wa utiwaji saini wa Mkataba wa Maridhiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rocket Tanzania Limited, Jumatatu, 4 Aprili 2022.

**********************

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshuhudia utiaji Saini Mkataba wa Utafiti wa Gesi ya Helia bym kati ya Kampuni ya Noble Helium Limited kupitia Kampuni yake Tanzu ya Rocket Tanzania Limited na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Utafiti wa Gesi ya Heliam katika maeneo mbalimbali nchini.

Utafiti huo, utahusisha maeneo manne tofauti ikiwemo eneo la Ziwa Nyasa, Ziwa Eyasi, Ziwa Rukwa pamoja na Ziwa Manyara ambapo mradi huo utaajiri wafanyakazi wake wote kutoka Tanzania na wafanyazi wasiozidi kumi watatoka nje ya nchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Kiruswa amesema viashiria vya uwepo wa gesi ya heliam katika maeneo mbalimbali ya nchi ni uthibitisho tosha unao onesha kubarikiwa kwa nchi ya Tanzania, kwani ni madini ambayo yanategemewa kuongeza Pato la Taifa kwa kuwa yanahitajika sana kwenye shughuli za uchumi wa kileo.

Pia, Dkt. Kiruswa ameishauri Kampuni ya Rocket Tanzania Limited kuishirikisha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kuwa ina taarifa nyingi za awali za uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) sababu shirika hilo linafanya shughuli za utafiti wa madini na lina vifaa vya kutosha vya utafiti.

"Naomba nichukue fursa hii kumpongeza Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake mazuri anayotupa sisi wasaidizi wake, anataka kuona mazingira ya uwekezaji nchini yanakuwa bora na ya kuvutia," amesema Dkt. Kiruswa.

Imeelezwa kuwa, uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki hususan kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, pia heliam hutumika katika teknolojia ya kutengeneza vifaa vya maabara, roketi, mitambo ya kinyuklia, vifaa vya elektroniki na vifaa vingine vingi.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Prof. william Anangisye amesema utiwaji saini wa mkataba huo wa maridhiano unadhihirisha hasa nia na nafasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuhudumia jamii.

Sanjali na hayo Prof.Anangisye amewaahidi uongozi wa Rocket Tanzania Limited Chuo hicho kitatoa ushirikiano wa karibu pale wanachuo watapokuwa wakitoa huduma katika utafiti wa Gesi ya Helium.

Pamoja na hayo amesema kuwa Chuo hicho kina nia ya kuongeza ubunifu na ugunduzi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za jamii ya kitanzania.

Nae Kaimu Amidi wa Shule Kuu ya Madini na Jiosayansi Dkt. Emmanuel Kazimoto amesema UDSM wameweza kupata kifaa maalumu cha kuchunguza gesi asili ikiwemo Helium (kinaitwa Mini Ruedi) ambacho ni kifaa cha pekee na ni kati ya vifaa adimu katika eneo la Afrika Mashariki ya kati na Kusini.

Amesema uwepo wa kifaa hicho kutafanya kuwa na uzoefu mkubwa Afrika katika utafiti wa rasilimali hiyo ya gesi ya Helium.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Rocket Tanzania Limited Bw. Justyn Wood amesema wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwani wamekuwa na makampuni watatu na wataalamu wa kutosha katika kuednesha program mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments