Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI GWAJIMA ATEMBELEA BANDA LA WATANZANIA MAONESHO YA KIMATAIFA YA MBOGA NA MATUNDA NCHINI UJERUMANI


***************************

Waziri anayehusika na masuala ya Wanawake na Makundi Maalum Mheshimiwa Dorothy Gwajima ametembelea banda la watanzania katika maonyesho makubwa ya kimataifa ya Mboga Mboga na matunda. Yuko nchini Ujerumani akihudhuria mkutano wa Gender wa G77.

 Waziri Gwajima ameipongeza sana Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Ujerumani kwa kufungua Fursa Hizi hasa kwa Wanawake wa Tanzania na kuomba Balozi nyingine ziendelee kufungua Fursa nyingi kwa makundi maalum na Wanawake.

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Tanzania huko UN-Geneva, Bi Hoyce Temu, alishiriki katika maonyesho hayo pia kwa mwaliko wa Balozi wa Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Uswisi ilipo UN.

Post a Comment

0 Comments