Ticker

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA CCM RAIS SAMIA ATEMBELEA OFISI ZA CCM MKOA WA TABORA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan leo Jumatano tarehe 18 Mei, 2022 ametembelea ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Ndg Hassan Mwakasubi akimkaribisha Ndg Samia Suluhu Hassan alimueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi mkoani Tabora na wananchi kwa ujumla wanaridhishwa na utendaji wa serikali anayoiongoza katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

"Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora. Haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali, tunakushukuru sana na tunakukaribisha Tabora." alisema Ndugu Mwakasubi.

Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza tarehe 17 Mei, 2022 na ataihitimisha tarehe 19 Mei, 2022 kwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamati ya Siasa ya MKoa (CCM) kwenye Ofisi za chama hicho mkoani Tabora leo jumatano Mei 18, 2022 ,mara baada ya kutembelea ofisi hizo, ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Wageni kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Tabora leo jumatano Mei 18, 2022 ,mara baada ya kutembelea ofisi hizo na kufanya Mazungumzo na Kamati ya Siasa ya mkoa huo.


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya MKoa wa Tabora wakimsikiliza Mwenyekiti wao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao,Mwisho kulia ni Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Taifa,Shaka Hamdu Shaka

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu akiwasalimia na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Tabora,mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Chama hicho leo,Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe,Balozi Batilda Buriani,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, Shaka Hamdu Shaka pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Ndugu Hassan Mwakasubi.

Post a Comment

0 Comments