Ticker

6/recent/ticker-posts

OTHMAN MASOUD OTHMAN:UBUNIFU UONGEZA KASI NA UFANISI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAENDELEO

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda wakikagua mabanda mbalimbali wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,akizungumza wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda ,akielezea umuhimu wa maonyesho hayo wakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga,akizungumza wakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Eliamani Sedoyeka,akizungumzawakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumzawakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. ............................................ 

Na Zena Mohamed,Dodoma.

 MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othman amesema Serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zinatambua umuhimu wa kuandaa mazingira yatakayowezesha kuibua ubunifu miongoni mwa Watanzania kwa lengo la kutumia ubunifu huo na teknolojia mbali mbali kuongeza kasi na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo. 

Othman amesema hayo jijini hapa leo wakati akiongea katika hafla ya ufunguzi wa wiki ya Kitaifa ya ubunifu na mashindano ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU)kwa mwaka huu kwa niaba ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi ambapo amesema, malengo ya Serikali zote mbili ni kuweza kuibua, kutambua na kuendeleza ubunifu na teknolojia hapa nchini na kuhamasisha matumizi yake katika kutatua changamoto mbali mbali zinazotukabili katika masuala ya kijamii na kiuchumi. 

"Kwa hivyo, hatua hii ya kuanzishwa kwa Mashindano ya Kimataifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yanayokwenda sambamba na Maadhimisho ya wiki ya Ubunifu tunayoyafungua leo, ni kielelezo cha jitihada za Serikali katika kuendeleza ubunifu,"amesema. 

Amesema Kupitia shughuli hiyo, wabunifu na wavumbuzi chipukizi nao wanapata fursa ya kutambulika na kuonesha kazi na vipaji vyao sambamba na kujifunza zaidi kwa wenzao wenye uzoefu na waliobobea. ".

Natoa shukurani zangu za dhati kwa uongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kunialika niwe Mgeni rasmi katika shughuli hii,naishukuru sana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuona umuhimu wa kuiandaa shughuli hii ambayo ina umuhimu mkubwa katika kufikia malengo ya Serikali zetu ya kuhamasisha na kushajiisha ubunifu ili iwe chachu ya kuongeza kasi na ufanisi katika sekta zote za maendeleo nchini.

 "Kwa hakika, nimeridhika na kutiwa moyo sana na mambo mbali mbali niliyoyaona wakati nikiyapitia mabanda ya maonesho hivi punde yakionesha hatua kubwa iliyofikiwa katika ubunifu wa bidhaa tafauti na utoaji huduma kwa kutumia teknolojia mbali mbali, "Nimefurahishwa na ubunifu wa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo: “Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu.” 

Ni dhahiri kuwa kauli mbiu hii inalenga kuwahamasisha Watanzania katika ngazi mbali mbali kufanya jitihada za kubuni utengenezaji wa bidhaa na kutumia teknolojia zenye kuchangia ukuaji wa uchumi hasa wa viwanda na kufikia hatua ya maendeleo endelevu,"amesema. 

Ameeleza kuwa hatua hiyo, ina mchango muhimu katika kufikia dhamira ya Serikali zote mbili ya kuimarisha uchumi na kuongeza fursa nyingi zaidi za ajira nchini. 

Ametaja Matarajio ya Serikali kuwa ni kuwa na ubunifu na teknolojia zinazoibuliwa na wabunifu na wagunduzi nchini, zitaongeza tija katika uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda, kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa pamoja na kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma katika nyanja mbali mbali.

 "Kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa mchango wa ubunifu na teknolojia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ninayoiongoza, tumekuwa tukifanya jitihada mbali mbali kwa lengo la kuhamasisha na kuendeleza ubunifu na teknolojia katika sekta ya umma zikiwemo taasisi za Serikali pamoja na Sekta binafsi,"amesema. 

"Tunafanya hivyo kwa kuamini kwamba ubunifu pamoja na kufanya tafiti mbali mbali zenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto tulizonazo ni vichocheo muhimu vya maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii kama ilivyobainishwa katika mipango yetu mikuu ya Maendeleo Tanzania Bara na Zanzibar na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020,"amesema Othman. 

Amesema Serikali zote mbili zimeazimia kujenga uwezo wa ndani kwa kuendelea kuwekeza katika rasilimali watu, miundo mbinu na vifaa vya kisasa vya utafiti na ubunifu pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Taasisi za Sayansi na Teknolojia pia sekta ya viwanda.

 Pamoja na hao amesema matunda ya jitihada za Serikali, katika utekelezaji wa malengo hayo na hatua zinachukuliwa yote yanabainika kupitia Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambapo jumla ya wabunifu wachanga 2,785 wameweza kuibuliwa mwaka huu.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,amevitaka vyuo vya elimu ya juu nchini kujiimarisha katika utafiti ili kupata maendeleo kwenye ugunduzi na ubunifu wa teknolojia zitakazosaidia Tanzania kupiga hatua zaidi.

 Mhe.Othman ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 

Amesema kuwa vyuo vikuu kazi yao ya msingi ni utafiti na kutaka kujiimarisha kwenye eneo hilo na kuwa na sera bora za tafiti ambazo zitasaidia na kuchagiza wabunifu na wagunduzi kwa kulinda haki zao na kufaidi matunda ya kazi zao.

 "Natoa wito kwa Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar kuandaa mikakati maalum ya kulinda kazi mbalimbali za ubunifu”amesema Mhe.Othman 

Mhe.Othman amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wiki hii na ndio maana maonesho haya yanafanyika ili kuendelea kuibua na kukuza vipaji tunapaswa kufanya maonesho naamini itatusaidia kuongeza kasi ya maendeleo kwa taifa. 

Aidha amesema kuwa serikali zote mbili zimeazimia kujenga uwezo wa ndani wa kuendelea kuwekeza katika rasilimali watu, miundombinu na vifaa vya kisasa vya utafiti na ubunifu pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Taasisi za Sayansi na Teknolojia na sekta ya viwanda. 

”Serikali zote mbili ya Muungano na Zanzibar zinatambua umuhimu na mchango wa ubunifu na teknolojia katika kurahisha na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za mbalimbali za kiuchumi na kijamii.”amesema Mhe.Othman 

Ameongeza kuwa ubunifu ukitumika vyema ni nyenzo na kichecheo muhimu cha maendeleo ya haraka katika sekta za huduma, jamii na uzalishaji na ndio maana Serikali inaendeleza bunifu hizo. 

“Serikali itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha na kitaalamu COSTECH, ili iweze kusaidia zaidi shughuli za utafiti na ubunifu nchini kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Mhe.Othman Pia Makamu wa Rais amepata fursa ya kutembelea na kujionea bunifu mbalimbali zilizopo katika mashindano hayo na kuvutiwa na bunifu hizo. 

Hata hivyo Mhe.Othman ameishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa Maonesho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa mwaka huu wa 2022 huku ikiwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa maendeleo endelevu” 

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda amesema Taasisi tofauti tofauti 50 pamoja na wabunifu 26 ambao bunifu zao zimefikia hatua ya kuingia sokoni na kuanza kutumika zimeshiriki katika maeonesho hayo. Ambapo amesema wabunifu 862 walijisajili kwa mwaka huu na wabunifu 86 bunifu zao zitashindanishwa ili kupata washindi.

Post a Comment

0 Comments