Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI BASHUNGWA APONGEZA ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA WATUMISHI NCHINI


*************************

Angela Msimbira SIKONGE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 23.3.

Akitoa salam za Ofisi ya Rais-TAMISEMI leo tarehe 18 Mei, 2022 kwenye uzinduzi wa barabara Tabora – Koga – Mpanda yenye urefu wa kilometa 342.9, uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Mkoani Tabora Mhe. Bashungwa amesema asilimia 75 ya watumishi wanatoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo amemuahidi Rais kufanyakazi kwa weledi katika kuwatumikia wananchi.

Waziri Bashungwa pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge hadi kufikia asilimia 193 na kubadilisha mandhari ya eneo hilo.

Bashungwa anaendelea kufafanua kuwa kwa upande wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 1.1 na shilingi milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya.

Amesema kwa upande wa ujenzi wa kituo cha afya Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Tuturo na kwa upande utatuzi wa changamoto za ujenzi wa nyumba za waalimu nchini katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 55.57 kwa ajili ya ujenzi huo

Bashungwa amesema kwa upande wa ujenzi wa jingo la utawala Serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 700 na katika bajeti ya mwaka 2022/2023 zimetengwa shilingi milioni 600 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la utawala ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la anuani ya makazi na kujitokeza kuhesabiwa ili serikali iweze kuwatambua na kuweza kutoa huduma bora kulingana na takwimu zilizopo.

Post a Comment

0 Comments