Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA NYONGEZA YA MISHAHARA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipopokea taarifa ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara kwa watumishi kutoka kwa timu ya watalaamu iliyokuwa ikiiandaa na ataiwasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wowote. Tukio hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 10, 2022.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

***************************

*Aahidi kuikabidhi kwa Mheshimiwa Rais Samia wakati wowote

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara ya watumishi kutoka kwa timu ya wataalamu iliyokuwa ikiyaandaa kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amepokea taarifa hiyo leo usiku (Jumanne, Mei 10, 2022) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Kikao hicho kiliwahusisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi pamoja na Makatibu Wakuu wa wizara hizo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema taarifa hiyo imeonesha kwamba maandalizi ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara yameshakamilika na kwamba wakati wowote atayawasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia ambaye atautangazia umma mabadiliko hayo yanayotarajiwa Julai mwaka huu.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Jumapili Mei Mosi 2022 aliwahikikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.

Post a Comment

0 Comments