Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA MBILI ZAPONGEZWA KWA USHIRIKIANO NA KULETA TIJA.


******************************

Na Hamida Kamchalla, Tanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amezipongeza Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Habari, Tekinolojia ya Habari kwa kushirikiana na kufanya vizuri katika utendaji wao na kufanikisha Wizara hizo kuleta tija kwa serikali.


Waziri Bashungwa ameyasema leo wakati akifunga kikao kazi cha Maofisa wa Habari, Mawasiliano na Mahusiano ya serikali kilichofanyika jijini Tanga kwa siku tano


"Naweza kusema kwamba hili ni jeshi ambalo serikali yetu inalitegemea sana katika kuhabarisha umma, kwahiyo tuendelee na ushirikiano huu mzuri kwa manufaa makubwa ya nchi yetu" amesema Bashungwa.


"Na nitahakikisha kwamba hizi halmashauri 85 ambazo hazina maofisa habari kati halmashauri zote 184 nchini na Mikoa minne ambayo haina maofisa habari, kati ya Mikoa 26zinapayiwa maofisa habari, lakini Mamlaka nyingi za serikali za mitaa hatujanunua vifaa vya kutosha na vinavyofaa kwa ajili ya kitengo cha habari" amesema.


Hata hivyo Bashungwa ameweka msisitizo kwamba kwasasa kitengo cha habari kinategemewa kwa kiasi kikubwa kutangaza kwa msisitizo habari za anuani ya makazi pamoja na sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments