Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI WA UTALII LYDIA AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KWA KUANZISHA MBIO ZA MARANGU NATURE WALK RIDE&RUN

BALOZI wa Utalii nchini Lydia Lukaba akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza mbio za Marangu Nature Walk Ride&Run zenye lengo la kutangaza utalii wa ndani kulia ni Afisa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya.
BALOZI wa Utalii nchini Lydia Lukaba akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza mbio za Marangu Nature Walk Ride&Run zenye lengo la kutangaza utalii wa ndani kulia ni Afisa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya na kushoto ni Fredy Moshi kutoka Ndoro Water Fall
Afisa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari kushoto ni Fredy Moshi kutoka Ndoro Water Fall
Fredy Moshi kutoka Ndoro Water Fall akizungumza

Meneja wa Hotel ya Hosea Inn Marangu Dues Masawe akizungumza

*******************

NA OSCAR ASSENGA,MOSHI.

BALOZI wa Utalii nchini Lydia Lukaba ameunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu za kutangaza utalii nchini kwa kuanzisha mbio za Marangu Nature Walk Ride&Run zenye lengo la kutangaza utalii wa ndani

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Marangu Balozi Lydia alisema licha ya kuzitumia kutangaza utalii wa ndani lakini pia watachangia taulo za Kike kwa ajili ya watoto wa kike ambao hawana uwezo kwa kupatiwa msaada huo.

Alisema mbio hizo ambazo zitakwenda sambamba na matembezi zitakuwa endelevu na zitafanyika Julai 10 mwaka huu na zitaanzia Marangu Mtoni yatakuwa ya kilomita 50,21 mara mbili na kilomita 40 za baiskeli na Kilomita 5.

Balozi Lydia ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Conservation Marathon alisema mbio hizo zitapita eneo la Kinukamori Water fall na kilomita 10 zitakwenda Ndoro Water falls wakati zile za Kilomoita 21 zitaanza kinapa na kwenda Mandara na kumalizika Marangu mtoni kwa Hosea.

Alisema katika mbio hizo wanategemea kuwa na vyakula vya asili,vinywaji vya asili mbege na kwenye vituo vyao vitakuwa na vyakula vya kichaga ni wakati mzuri wa kupata uzoefu lengo mbali na kutangaza utalii na wameshirikisha shule mbalimbali za Msingi na sekondari .

Balozi huyo alisema wamefanya hivyo wakiamini kwenye utalii ni vizuri wakihusisha watoto wadogo waweze kujua utalii tokea wakiwa chini huku akiomba serikali iweze kuangalia suala hilo kwa kuanzia kufundisha utalii kuanzia shule za Msingi.

“Tumeona tutangaze utalii kupitia mbio kwani pia ni tiba na kumekuwa na mwamko mkubwa kwani watanzania hushiriki mbio mbalimbali kupitia hilo tunawakaribisha watanzania”Alisema ,

“Lakini pia lengo kuanzisha mbio hizo ni kuunga mkono juhudi ambazo zimeanzishwa na Rais Samia kwenye kampeni yake ya kutangaza vivutio vya utalii nchini”Alisema

Alisema Rais amefanya jambo kubwa na nzuri hivyo wao kama wadau wa utalii wameona watumie fursa ya kuanzisha mbio hizo kwa lengo la kuhakikisha wanakwenda sambamba na malengo ya Rais Samia.

Awali akingumza Afisa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro Vitus Mgaya alisema wameunga na Balozi wa Utalii Lydia ambaye amehamasisha kuandaa mbio za watu kutembelea ndani ya hifadhi kuendesha baiskeli na shughuli nyengine za utamadhu wao kama hifadhi wanamuunga mkono kwa juhudi zake na watamsaoti na watashirikisha watu wengine.

“Mbio hizo ni nzuri kwa sababu zitakuwa zinatangaza utalii na hivyo kuwafanya watanzania waweze kufahamu vivutio vyao na kuweza kutangaza utalii waje waungane Marangu tunawakabisha watanzania wote wajiandikishe”Alisisitiza.

Naye kwa upande wake Meneja wa Hotel ya Hosea Inn Marangu Dues Masawe alisema wazo aliloamua kulifanya Balozi Lydia kwa mbio hizo ni nzuri na watamuunga na kuwataka watanzania wamsapoti .

Hata hivyo kwa upande wake Fredy Moshi kutoka Ndoro Water Falls ambao wanaojishughulisha na uhifadhi wa mazingira na kuotesha miti alisema mbio hizo za zitapita kwenye eneo lao na wamejiandaa vizuri na wana mshukuru Lidya huku wakiwaomba wadau wengine wamsapoti wakiwemo Kinapa na Tanapa.

Post a Comment

0 Comments