Ticker

6/recent/ticker-posts

BONANZA LA WAFANYAKAZI CRDB KANDA YA KASKAZINI LAZINDULIWA

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akiongea na wafanyakazi hao wakati akifungua Bonanza la michezo kwa matawi ya benki ya CRDB Kanda ya kaskazini, katika uwanja wa Mkwakwani likiwa na lengo la kuwahamasisha kujali na kuimarisha kinga za mwili.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akipatiwa huduma ya matibabu, kupima Afya kabla ya kufungua Bonanza la michezo kwa matawi ya benki ya CRDB Kanda ya kaskazini, katika uwanja wa Mkwakwani likiwa na lengo la kuwahamasisha kujali na kuimarisha kinga za mwili.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB kanda ya kaskazini wakiwa na mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa wakifanya mazoezi mara baada ya Bonanza lao kufunguliwa rasmi.

******************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


WAFANYAKAZI wa benki ya CRDB Kanda ya kaskazini, matawi ya Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro wamefanya bonanza la michezo matawi katika uwanja wa Mkwakwani likiwa na lengo la kuwahamasisha kujali na kuimarisha kinga za mwili.


Bonanza hilo pia limeambatana na zoezi la kupima Afya kwa magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ikiwemo kisukari.


Akifungua bonanza hilo mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa amewataka wafanyakazi hao sambamba na jamii yote kuwa ujumla kuwa na desturi ya kupenda kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa pia ni sehemu ya kaimarisha utimamu wa mwili na kuondokana na msongo wa mawazo.


"Wafanyakazi wengi kwenye maisha yetu tumejiwekea mtindo wa kwenda ofisini kurudi nyumbani kula na kulala tu, hali ambayo ni hatari kwa afya zetu, miili yetu imekuwa ni dhaifu na kinga zimeshuka, niwasihi sana tupende kuweka ratiba zetuza kufanya mazoezi itatusaidia sana" alisema Mgandilwa.

Michezo mbalimbali imefanyika katika uwanja huo ambapo tawi la Wilaya ya Korogwe mkoani hapa limeibuka mshindi wa jumla kwenye zoezi la kuvuta kamba wakiondoka na kitita cha shilingi laki mbili, kufukuza kuku kwa wanaume tawi la Handeni wamejinyakulia 50,0000, kwa wanawake ikienda tawi la tawi la Lushoto nalo pia kuondoka na 50,000.


Tawi la Handeni lilizidi kuwaburuza wafanyakazi kutoka matawi mengine baada ya kushinda kwenye mchezo wa kufukuza kuku na kukimbia kwa magunia yote miwili wakijizolea shilingi 100,000 na kwa upande tawi la Tanga na Lushoto wakipewa kila mmoja 50,000.


Katika mchezo wa mpira wa miguu matawi ya Handeni, Tanga na Lushoto yaliunda timu moja na hatimaye walifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi 150,000 baada ya kuwafunga kwa mikwaju ya penati wenzao kutoka matawi ya Tanga na Korogwe .


Akizungumza meneja wa kanda ya kaskazini Chiku Issa alisema kuwa "tukiwa na wafanyakazi wenye afya bora tutaweza kuwahudumia wateja wetu vizuri, unaweza ukawa umaonekana kuwa uko vizuri kumbe kiafya bado una changamoto kuwahiyo tunawajibika kuhakikisha kwamba katika kazi zote tunazofanya ndani ya benki mfanyakazi afya yake lazima iwe ni namba moja".

Post a Comment

0 Comments