Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YATOA MAFUNZO YA UDHIBITI SUMUKUVU KWENYE MAZAO WILAYANI NZEGA

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe.Ricardo Komanya akifungua mafunzo kuhusu Udhibiti wa Sumukuvu kwa Mzao ya Mahindi,Karanga pamoja na bidhaa zake kwa wafanyabiashara, Wazalishaji na Wasindikaji kutoka katika Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.

Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kuhusu Udhibiti wa Sumukuvu kwa Mzao ya Mahindi,Karanga pamoja na bidhaa zake katika Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora wakiwa kwenye mafunzo hayo.

**********************

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa mafunzo kuhusu Udhibiti wa Sumukuvu kwa Mzao ya Mahindi,Karanga pamoja na bidhaa zake kwa wafanyabiashara, Wazalishaji na Wasindikaji kutoka katika Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.

Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo leo Juni 6,2022 wilayani hapo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe.Ricardo Komanya amesema Sumukuvu imekuwa ikiathiri zaidi mazao ambayo ni sehemu ya chakula chetu hapa nchini hivyo basi tunapaswa kuzingatia mikakati ya kukabiliana na changamoto ya sumukuvu ili vyakula viendelee kuwa salama kwa muda wote.

Amesema kupitia mafunzo hayo ambayo TBS wameyakusudia kuyatoa kwa wahusika yatasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na sumukuvu na hivyo kuzalisha na kuuza bidhaa ambazo ni salama.

"Niwapongeze TBS kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania -TANIPAC kwa kutoa kipaumbele katika suala la kuelimisha jamii ya Wilaya ya Nzega juu ya usalama wa chakula hususan katika kudhibiti Sumukuvu ili kuweza kukabiliana na tatizo hili". Amesema Mhe.Komanya.

Post a Comment

0 Comments