Ticker

6/recent/ticker-posts

UFUNGUZI WA MDAHALO KWENYE KONGAMANO LA 13 LA KIGODA CHA MWALIMU NYERERE


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo kwenye kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Juni 8, 2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akifungua mdahalo katika kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Juni 8,2022 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza kwenye ufunguzi wa mdahalo katika kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Juni 8, 2022 katika Chuo Kikuu cha Dar es SalaamMwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Prof.Rwekeza Mukandala akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo kwenye kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Juni 8, 2022 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Florens Luoga (katikati) akiwa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda katika ufunguzi wa mdahalo kwenye kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika leo Juni 8,2022 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Baadhi ya wadau wakifuatilia ufunguzi wa mdahalo katika kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete amewataka vijana kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kujituma zaidi na kujifunza huku wakiendeleza ujamaa ambao aliusisitiza hasa katika kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo Juni 8,2022 wakati akifungua mdahalo katika kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema miongoni mwa maono ya Mwalimu Nyerere ilikuwa kuona Afrika inakuwa kimaendeleo na kumudu kujitegemea kiuchumi huku akiwataka vijana kutumia elimu yao kujikomboa kiuchumi.

Nae Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Prof.Rwekeza Mukandala amesema maarifa yanayitolewa katika Kigoda cha Mwalimu Nyerere yamedhamiria kuwajengea vijana kuwa na maisha ya kufanya kazi, kujituma na kujitolea.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye amesema yale mawazo yote yatakayowasilishwa katika kigoda hicho yatafanyiwa utaratibu ili kuweza kutolewa kitabu kimoja cha mwalimu nyerere ikiwa ni sehemu ya kumuenzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu Bw.John Kalage amesema falsafa ya Mwalimu Nyerere ilijikita katika kutokomeza ujinga na Taasisi ya Haki Elimu wakishirikiana na Kigoda cha Mwalimu Nyerere wamedhamiria kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inakidhi matakwa ya sasa.

Post a Comment

0 Comments