Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DK.MWINYI ASHIRIKI SWALA YA IJUMAA MIEMBENI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) leo ameshiriki katika swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar,iliyoswalishwa na Sheikh Iddi Muhsin Iddi kutoka Ofisi ya Muftiu Mkuu wa Zanzibar .[Picha na Ikulu] 08/Julai 2022.

Baadhi ya Waumini wa Dini ya kiislamu wakiwa katika Msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar wakisikiliza hutba ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar iliyosomwa na Sheikh Khalid Ali Mfaume (hayupo picnani), na swala ikaswalishwa na Sheikh Iddi Muhsin Iddi kutoka Ofisi ya Muftiu Mkuu wa Zanzibar .[Picha na Ikulu] 08/Julai 2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kulia) pamoja Viongozi wengine wakiitikia dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,(katikati) baada ya Swala ya Ijumaa ilyoswaliwa leo katika msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 08/07/2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiagana na Spika wa baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid (katikati) pamoja Viongozi wengine mara baada ya Swala ya Ijumaa ilyoswaliwa leo katika msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 08/07/2022.

Post a Comment

0 Comments