Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAHAKIKISHA KATIBA MPYA INAPATIKANA

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damasi Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam

***********

Na Magrethy Katengu

Serikali imesema licha ya kwamba wadau wanahitaji katiba mpya wameshauri wadau kuchukua baadhi mambo yaliyopo kwenye rasimi ya Jaji Joseph Warioba kwa kufanyia Marekebisho mapungufu na kuyaingiza katika katiba mpya yaendelee kutumika .

Akizungumza na waandishi wa Habari wa waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbalo amesema kutokana na kuwepo na Mapungufu kwenye katiba iliyopo ndio Maana Serikali imetoa wigo mpana kwa Asasi za kirahia na wadau mbalimbali kuweza kujadili ili kuweza kuirebisha na kupata Katiba Nzuri zaidi isileta malalamiko kwa baadhi ya watu .

"Katiba hii ni Nzuri inafaa ila ina mapungufu, hata katiba ya Marekani inayo mapungufu lakini huwa inafanyiwa Marekebisho siyo kupita kila kona na mabango kudai katiba mpya Sasa ni wakati WA kukaa meza Moja kuunda katiba isiyoegemea au kutetea upande wowote ". Amesema Dk Ndumbalo

Dkt. Ndumbalo aliongeza kwakusema kumekuwepo na mijadala kuhusu katiba mpya kudai katiba mpya hivyo serikali ya awamu ya sita itahakikisha katiba mpya inapatikaba kwa kufanyia marekebisho katiba rasimu ya katiba ya Jaji Warioba Ili kuleta mlengo nzuri yenye uliokusudiwa

Waziri amesema matika mchakato huo Serikali imekuwa ikishirikiana vizuri wadau mbalimbali kutoka nyanja zote ikiwemo Asasi za kirahia vyama vya kisiasa dini makundi mbalimbali bila ubaguzi wowote .

"Katiba haikuwekei chakula mezani ila inakupa Uhuru kwa hiyo suala kuheshimu katiba ni kila mtu". Aliongeza Dkt. Ndumbalo.

Post a Comment

0 Comments