Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAAGIZA MIFUKO YA NSSF NA PSSSF KULIPA WASTAAFU STAHIKI ZAO***************************

NA MAGRETHY KATENGU

Serikali kupitia Wizara Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira ,Vijana na Watu wenye Ulemavu imeagiza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF )na Mfuko wa pensheni kwa Wastaafu (PSSSF )kuhakikisha wanawalipa Wastaafu wote ikiwemo wanaodai kiinua mgongo,fidia, mafao na Waliopunjwa.

Agizo hilo amelitoa leo Dar es salaam Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira,Vijana na Watu wenye Ulevumu Prof Joyce Ndalichako katika Mkutano alioitisha na kuonana na wastaafu wa Mkoa wa Dar es salaam Kwa lengo la kusikiliza malalamiko yao ,ambapo amedai kuwa tangu ameingia kwenye Wizara hiyo takribani miezi sita amebaini wastaafu wengi wamestaafu lakini bado hawajalipwa stahiki zao na wanaishi maisha magumu hivyo waje na vielelezo ili wafanyiwe mchakato wa kulipwa.

"Wastaafu hawa wanaodai madai yao wapo katika makundi tofautitofauti ikiwemo mapunjo ambapo mafao ya mtu yamekokotolewa kwa kutumia mshahara ambao ni mdogo kuliko mshahara halisi wa mfanyakazi alipostaafu na kusababisha mafao ya mkupuo anayopewa ni kidogo kuliko ilivyotakiwa"amesema Profesa Ndalichako.

Hata hivyo amesema kwamba amefuatilia na kubaini kuwepo kwa kesi za wastaafu ambazo ziko wazi nakwamba suala lililopo nikwenda tu kurekebishiwa mapunjo yao na kulipwa kwa kuzingatia mshahara wake wa mwisho ,nakusisitiza wastaafu hao warudishiwe stahiki zao zote walizokuwa wanapunjwa.

Aidha amesema kwamba kuna baadhi ya Wastaafu vikokotoo vyao viko sawa lakini walikuwa hawana Elimu juu ya Vikokotoo hivyo,ambapo wamepatiwa Elimu na kujiridhisha kwamba hawajapunjwa mafao yao.

Sambamba na hayo Waziri Ndalichako amesema kumekuwa na makosa ya kiutendaji kutoka kwa baadhi ya watendaji wa mifuko ya pensheni kutokusikiliza malalamiko ya wastaafu wanaokuja kudai stahiki zao hivyo ameagiza watendaji hao kuacha tabia hiyo kwani wao ni watishi wa Umma.

Kwa upande wake Kassim Mafanya alikuwa Mtumishi Chuo cha Askari Magereza Ukonga amesema anashukuru kupata nafasi kusikilizwa kwani wastaafu wengi wamekuwa wanaishi kwa msongo wa mawazo na maisha yao hayaeleweki hawajui kesho yao wamekuwa wakiahidiwa kupata nyongeza lakini hakuna kinachoendelea wengine wanafariki bila hata ya kufaidi chochote kutokana na jasho lao.

Naye Mtumishi Mstaafu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Chuki Kashaija mwenye ulemavu wa miguu amesema alianza kazi tangu mwaka 1973 nakustaafu mwaka 2014,ambapo amesema mpaka sasa hajapata mafao yake takribani miaka 8 sasa.

Wizara hiyo imepanga kufanya zoezi la kusikiliza malalamiko ya Wastaafu nchi nzima ikiwa ni Utekelezaji wa agizo la Mhe Rais Samia Suluhu Hassan aliloliagiza siku ya wafanyakazi Duniani( Mei mosi) iliyofanyika mwaka huu Jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments