Ticker

6/recent/ticker-posts

TANESCO TANGA YAWAONYA WANAOHARIBU MIUNDOMBINU

Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel Kimario akizungumza na waandishi wa habari leo .
Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel Kimario akizungumza na waandishi wa habari leo .




Na Oscar Assenga, Tanga

SHIRIKA la Umeme nchini Tanesco limewaonya wananchi wenye tabia za kuhujumu miundombinu kuacha mara moja tabia hizo kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani na kifungo.

Onyo hilo lilitolewa na Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel Kimario wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu changamoto zinazosababisha ukosefu wa umeme kutokana na uharibifu na hujuma kwenye miundombinu ya shirika hilo.

Alisema vitendo hivyo vinafanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu na kusababisha shirika kutumua fedha nyingi kurudisha huduma na shughuli za umeme katika hali ya kawaida na pia kupelekea wateja kukosa huduma hiyo na kuzorotesha shughuli za kiuchumi za kila siku.

“Lakini kutokana na gharama kubwa ambazo zinatumika kurudisha huduma kutokana na uharibifu shirika linaingia gharama kubwa na hivyo kupunguza kasi ya usambazaji wa umeme kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme”alisema

Hata hivyo aliomba wananchi wawape ushirikiano kwa kuwafuchua wananchi ambao wamekuwa wakihujumu miundombinu ya shirika hilo ikiwemo kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili waweze kuchukuliwa hatua na kuhakikisha miundombinu yao inakuwa salama na huduma inapatikana ipasavyo.

“Tumekuwa tukifanya operesheni kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha huduma inapatikana na pale ambapo mwananchi anabainika amehujumu miundombinu kunawachukuliwa hatua”Alisema

Aidha alisema hivi karibu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kulitokea hujuma kwenye maeneo yao na walifanikiwa kuwamata baadhi ya watuhumiwa mashauri yao yapo mahakamani na mmoja wapo alifunguliwa shauri la uhujumu uchumi namba 1 la mwaka 2022 na limemalizika na mtuhumiwa amehukumiwa kwenda Jela miaka 20.


Alisema hatua ya kukamatwa mtuhumiwa huyo na wengine ambao mashauri saba yanaendelea kwenye mahakama za wilaya za Handeni,Lushoto na Tanga mjini ambapo kati ya hayo mawili yametolewa hukumu ni kutokana na operesheni ambayo wameifanya kushirikiana na vyombo vyengine vya usalama na kufanikiwa kuwakamataa.

Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa Mahamud Hamisi shauri hilo lilimalizika Julai 12 mwaka huu huku akitoa rai kwa wananchi kulinda miundombinu na kuitunza ikiwemo kutambua kwamba ni jukumu la watu wote kuilinda na wale wanaofanya hujuma kuacha kufanya hivyo kwani hawapo tayari kuona watu wachache wanahujumu muindimbiu hiyo .


Post a Comment

0 Comments