Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAFUNGUA RASMI TAWI LAKE WILAYANI LUSHOTO, TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba (katikati) kwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori (wapili kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022. wengine pichani ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Suleiman Mzee (wapili kulia), Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Kalist Lazaro (kulia), pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Lushoto, John Mtani.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba (kulia) kwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori wakigungua kitabaa kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto mkoani Tanga, jana Agosti 29, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba ameongoza sherehe za ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo wilayani Lushoto na kuwataka wananchi wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zitolewazo na Benki hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mgumba alisema "Wakazi wa Lushoto na vitogoji vyote vinavyozunguka wilaya hii, niwape rai ya kuitumia benki hii kama chachu ya maendeleo wilayani hapa, haswa katika kutumia huduma za kibenki lakini pia kujipatia mikopo mbalimbali iltolewayo na benki hii ya CRDB".

Aidha, Mgumba aliendelea kusema "Serikali kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuwawezesha wananchi kiuchumi ndio maana inasogeza huduma zikiwamo za kifedha jirani yenu. Kila mmoja aangalie fursa zilizopo kukuza uchumi wake," alisisitiza.

Kwa upande wa Afisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema, wakazi wa Lushoto na vitongoji vyake sasa wanayo fursa ya kulitumia tawi hilo ambalo kwa sasa limeondoa changamoto ya kufuata huduma za kibenki wilayani Korogwe, kwa kusogeza huduma kwa wananchi na leo tumefika Lushoto,

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori alisema, wataendelea kushirikiana na Serikali kufanikisha shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini hasa katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa zitolewazo na benki ya CRDB ikiwemo mikopo nafuu ya kilimo ambayo kwasasa riba yake ni asilimia 9 tu. Hivyo aliwataka wanalushoto kuchangamkia fursa hiyo na kuhakikisha wanainua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia katika vikundi na kufanikisha miradi ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments